December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwandishi wa habari Dk.Tumain Msowoya akipokea fomu ya kuwania ubunge viti maalum kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (Kushoto),kutoka kwa Katibu wa UWT Mkoa wa Iringa, Angela Milembe katika Ofisi za CCM mkoani humo.

Wanahabari wajitosa kuwania nafasi za Ubunge na Udiwani

Na Penina Malundo,timesmajira ,Online

WAANDISHI wa Habari wamejitosa katika kuwania nafasi za Ubunge na udiwani katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Mpiga picha wa Gazeti la Majira Heri Shabani (KUSHOTO),akikabidhiwa fomu ya nafasi ya Udiwani Kata ya Tabata kutoka kwa Katibu wa CCM ,Haruna Alphonce leo jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa waandishi hao ni pamoja na Mwandishi wa habari nchini Tanzania, Dk Tumain Msowoya amechukua fomu ya kuwania ubunge viti maalum kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Iringa.

Mwingine ni Mpiga Picha wa Gazeti la Majira,Heri Shabani nae amejitosa katika kiny’anganyiro cha kuchukua fomu na kuwania nafasi ya udiwani katika kata ya Tabata.

Dk Tumain ambaye ni Afisa Habari wa Kampuni ya Kuzalisha nguzo za Umeme ya Qwihaya na Heri shabani ambae ni mpiga picha wa Gazeti la Majira wamekabidhiwa fomu hizo leo Jumanne tarehe 14 Julai 2020 na Makatibu wa maeneo yao husika.

Dk.Tumain amekabidhiwa na Katibu wa UWT Mkoa wa Iringa, Angela Milembe katika Ofisi za CCM mkoani huku Heri akikabidhiwa na Katibu wa CCM Kata Tabata Haruna Alphone