*Waahidi kuwa mabalozi wa barabara katika jamii
Judith Ferdinand Timesmajira Online-Dodoma
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kisasa wametembelea banda la Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) katika maonesho ya Nane Nane, yanayofanyika kitaifa viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Wakiwa katika banda hilo,Agosti 7,2025,wamepata elimu na mafunzo kuhusu kazi na mchango wa RFB katika sekta ya kilimo.
Wanafunzi hao, wameeleza kufurahishwa na elimu hiyo na kuiopongeza bodi hiyo kwa utendaji kazi wake katika kuhakikisha matengenezo na maboresho ya miundombinu ya barabara yanafanyika ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku wakiahidi kwenda kuwa mabalozi wa masuala ya barabara.
Sanjari na hayo Bodi hiyo imetoa wito kwa wananchi wote kutembelelea banda la bodi hiyo kwenye Hema la Serikali namba 4, banda namba 13 Nzuguni-Dodoma,ili waweze kupata elimu ya namna inavyofanya kazi.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi