November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi 7176, kufanya mtihani wa taifa 

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza 

Jumla ya watahiniwa 7176 waliosajiliwa  Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, wataungana na wenzao nchini,kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2024 utakaoanza 11 hadi 29 Novemba 2024.

Kati ya watahiniwa hao watakapofanyia mtihani  huo,katika Halmashauri hiyo wavulana ni 3467 na wasichana ni 3709.

Hayo yamebainishwa Novemba 9,2024,katika taarifa iliotolewa na  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Violencea Mbakile,alisema  watahiniwa 6989 ni wa shule.Kati yao  wasichana 3588 na wavulana  3401. 

Huku watahiniwa  187 ni wa kujitegemea,kati yao wavulana  66 na wasichana 121.Na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina jumla ya vituo 60 vilivyosajiliwa kuendesha mtihani wa taifa wa kidato cha nne (CSEE) kwa mwaka 2024.

 “Kati ya vituo hivyo 48 ni vya watahiniwa wa shule na vituo 12 ni vya watahiniwa wa kujitegemea.Mkurugenzi Ummy Wayayu, kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,amewatakia kila la kheri watahiniwa wote wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2024 na kuwakumbusha kuzingatia na kufuata taratibu zote za mitihani ili waweze kuhitimu salama,”.