Na Irene Clemence,TimesMajira Online, Dar
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya wanafunzi 47,305 wa mwaka wa kwanza wa masomo 2020/21 unaotarajia kuanza hivi karibu ambapo jumla sh. bilioni 150.03 zimetegwa kwa ajili yao.
Akitagaza orodha ya wanafunzi hao Jijini Dar es Salaam leo, Mkurungezi wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema kati ya wanafunzi 47,305, wanaume 26,964 sawa na asilimia 57.37 huku wanawake ni 20,341 sawa na asilimia 42.63.
Amesema HESLB tayari imeanza kupeleka fedha za wanafunzi waliopagiwa mikopo katika vyuo mbalimbali.
“Serikali imeishatupatia fedha na tumeanza kuzipeleka vyuoni lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wenye sifa wanazikuta fedha vyuoni ambako watasajiliwa na kupokea ili watimize ndoto zao,”amesema Badru.
Ameongeza kuwa wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza waliopagiwa mikopo kwa kuwa wanasifa zikiwemo kuwa mahitaji, wameomba kwa usahihi na wana udahili wa chuo kimoja.
Amesema kwa sasa wanafunzi wanatakiwa kupata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mikopo ya SIPA na kujiandaa kwenda vyuoni kwa ajili ya kujisajili.
Kwa taarifa zaidi soma Gazeti la Majira kesho
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi