Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAFANYABIASHARA Nchini wametakiwa kusajili majina ya biashara na makampuni yao Ili waweze kutambulika kisheria lakini kufanya biashara zao kihalali .
Akizungumza jijini Dodoma katika maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini kwenye banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Ndeyanka Mbowe amesema pia kufanya hivyo watakuwa wametimiza matakwa ya Sheria .
Amesema,Moja ya faida za kujisajili kwa wafanyabiashara na makampuni ni pamoja na kutambulika na Mamlaka husika,kupata huduma za kifedha katika mabenki kama mikopo na kupata tenda Serikalini .
“Kwa wale wanaofanya shughuli za viwanda wakajisajili maana bila kufanya hivyo ni kosa kisheria .”amesema Ndeyanka
Amesema kwa wale wanaofanya biashara zilizopo katika kundi A ambazo zina sura ya kitaifa ,kimataifa na zinasimamiwa na Sera Maalum kama ukopeshaji fedha,biashara za utalii,kuingiza na kutoa mizigo ndani ya Nchi kujisajili ni jambo la muhimu.
Aidha amesema katika maonesho hayo wamekuwa wakitoa Elimu kuhusu BRELA lakini pia wamekuwa wakisajili majina ya biashara pamoja na makampuni kwa wateja wanaofika katika banda lao.
Kwa upande wake Mwanasheria wa BRELA Andrew Malesi amesema matumizi ya jina la biashara au kampuni bila kusajili yanaweza kusababisha hasara na mwingine asiyehusika kupata faida.
More Stories
Bunge lapitisha muswada wa Sheria za kazi,wanaojifungua watoto njiti waongezwa likizo ya uzazi
GreenFaith yatoa mapendekezo yake mkutano wa mission 300 kwa Wakuu wa nchi,Serikali za Afrika
Mwenyekiti UVCCM ataka wakandarasi kuwa na weledi ujenzi wa miradi