Na Joyce Kasiki,Timesmajira online Dodoma
VIONGOZI na wanachama wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi ya kugombea uongozi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), ngazi ya Mkoa na uwakilishi wa makundi maalum Kitaifa kwa maendeleo ya sekta ya mashirika hayo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Mwenyekiti kamati ya Mpito ya Kuratibu Uchaguzi wa Baraza hilo,Christina Ruhinda amesema kuwa uchanguzi unatarajiwa kufanyika Juni 11, mwaka huu katika eneo ambalo limeandaliwa.
Ruhinda amesema kuwa wagombea waliopita kutoka ngazi ya Wilaya moja kwa moja wamefuzu kushiriki katika uchanguzi ngazi ya Mkoa ili kupata mshindi mmoja kwa kila Mkoa atakayekuwa sehemu ya wajumbe wa Baraza hilo.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi Mkoa limeanza Juni 3 hadi 4 mwaka huu na kurudisha ni Juni 5 hadi 6 mwaka huu.
“Mchakato fomu za kugombea nafasi hii utaanza Juni 7 hadi 8 na zoezi la kampeni la kupiga kura ,kuhesabu kura, kutangaza matokeo na kupitisha washindi ambapo zoezi hili litafanyika katika eneo lililoandaliwa ambapo wagombea watanadi sera zao kwa wapiga kura katika kila mkutano wa uchanguzi,’ amesema Ruhinda
Aamesema kuwa Juni 11 kampeni, zoezi la kupiga kura, kuzihesabu , kutangaza matokeo na kupitisha washindi ambapo zoezi hilo litafanyika katika eneo lililoandaliwa.
Kwa mujibu wa kanuni 5 (a) (v), 5(b) (ii) na 5(c)(v) ya kanuni za uchanguzi za Baraza la
NaCoNGO, ya mwaka 2016 Baraza hilo linatakiwa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitatu.
Aidha Baraza la NaCoNGO limeanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 25 (1) cha sheria ya NGO’s sura ya 56 ya sheria za Tanzania, NaCoNGO ni chombo huru ambacho ni mwamvuli wa mashirika yasiyo ya Kiserikali zilizo sajiliwa Tanzania Bara.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba