December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanachama CCM )Mkoa wa Shinyanga wamempogeza Ndugai

Na Mwandishi wetu, Timesmajira online

ZIKIWA zimepita ni siku chache toka Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kujitokeza hadhari na kumuomba radhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM )Mkoa wa Shinyanga kupitia Mwenyekiti wa Mkoa huo Mabala Mlolwa wamempogeza Spika Job Ndugai na kueleza kuwa ameonesha ukomavu wa kisiasa, Uzalendo na utii kwa Chama Cha Mapinduzi CCM.

Mlolwa ameyasema hayo Jijini Dar Dar es salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Wanachama wa CCM Mkoa wa Shinyanga na Wananchi kwa ujumla .

Mlolwa amesema kauli zilizotolewa na Spika Job Ndugai ziliweza kusababisha taharuki katika jamii hivyo kitendo cha kuomba radhi kimeonesha kutambua makosa yake .

Ameongeza kuwa Spika Job Ndugai ameonesha ujasiri kwa kuomba msamaha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na watanzania kwa ujumla ambapo kitendo hicho kimeonesha na kudhihirisha kwa Wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa ametambua kosa alilofanya.

“Nampongeza Spika Ndugai kwa kutambua kosa lake ameonesha uzalendo wa Chama cha Mapinduzi CCM ikiwemo ukomavu na ukongwe na chenye uzoefu wa Uongozi na demokrasia na viongozi kukubali kukosolewa na kukubali kujishusha na kutoka hadharani kwa unyenyekevu kuomba radhi na msamaha kwa watanzania pale wanapobaini wamekengeuka”alisema

Pia amesema kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na wanaCCM wanamuombea msamaha Spika Job Ndugai kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye ni amri Jeshi Mkuu pia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa kumsamehe kosa lake kama alivyoomba Mwenyewe hadhari kwa kutambua kuwa ni mkosaji.

Alibainisha kuwa umoja na Mshikamo utaendelea katika Chama cha Mapinduzi CCM na kueleza kuwa ndani ya Chama hicho hakuna mgawanyiko na kueleza kutokea kwa mambo kama hayo ni kukengeuka kwa binadamu

“Hakuna binadamu ambaye amekamilika kila mtu anamapugufu yake ..Chama chetu kipo imara, hakuna makundi na kipo imara”alisisitiza Mlolwa

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam.