April 3, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wana-CCM watakiwa kudumisha amani kuelekea uchaguzi mkuu

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, amewataka wanachama wa chama hicho kudumisha amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza jijini Arusha kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mongella amewahimiza wana-CCM kuwa makini na kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha vurugu.

Amesisitiza kuwa, huu ni wakati wa kuwa imara huku akieleza kuwa Tanzania ina heshima ya kipekee barani Afrika kutokana na utamaduni wake wa kudumisha amani na utulivu.