Na Mwandishi wetu, TimesMajiraOnline
Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidijitali nchini Tanzania, Tigo, leo imefanya kongamano la wanahabari kutoka vyombo vya habari vinavyotambulika ili kuungana na kuweka wazi mipango yake ya siku za usoni inayolenga kuchochea tasnia ya mawasiliano nchini Tanzania baada ya muungano ulioongozwa na Axian Telecom na mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Bw. Rostam Azizi na kupata taasisi iliyounganishwa ya MIC Tanzania PLC (Tigo na Zantel).
Mkutano huo ulielezea mipango kabambe ya ukuaji wa Axian Telecom ili kusaidia mageuzi ya kidijitali nchini Tanzania kwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili kuimarisha mtandao na ubora wa huduma wa taasisi iliyounganishwa ya MIC Tanzania plc.
Akizungumza katika KONGAMANO Hilo Mwenyekiti wa MIC Tanzania PLC, Bwn. Rostam Azizi alisema,
“Tunafuraha kukutana na wanahabari ili kuelezea mipango yetu ya baadaye kwa wateja zaidi ya milioni 14 kote nchini. Kufuatia uzoefu wa miongo kadhaa katika sekta hii, nimejitolea kutoa mwongozo wa kimkakati na uwakili muhimu kwa Tigo ili kupanua ufikiaji wa huduma za simu za mkononi za bei nafuu na kusukuma ushirikishwaji wa kidijitali kote nchini Tanzania kupitia uwekezaji mkubwa katika miundombinu yetu ya mawasiliano”.
Lakini pia akizungumza katika kongamano hilo hilo, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya AXIAN Telecom, Hassanein Hiridjee, alisema
“Uwekezaji wetu katika taasisi iliyounganishwa (Tigo na Zantel) utatusaidia kutimiza azma yetu ya kuwa mshirika wa mwisho-mwisho katika mageuzi ya kidijitali barani Afrika na kuongeza kasi zaidi ya ujumuishaji wa kifedha, kwa kutumia mtaji wa mafanikio ya huduma za kifedha za simu za mkononi za shirika lililounganishwa ili kuendeleza huduma za kawaida zinazokidhi mahitaji ya mteja wetu”.
Kwa kutumia utaalam wake hasa katika kusambaza teknolojia za hali ya juu na kuendeleza huduma za kifedha za simu za mkononi zenye mafanikio, AXIAN Telecom na Bw. Rostam Aziz wana nia ya kuwezesha mfumo ikolojia wa mawasiliano nchini Tanzania kwa lengo la kuhakikisha matumizi bora zaidi kwa wateja na wafanyakazi.
Mipango inaendelea kwa timu zilizounganishwa kuhamia kwenye jengo refu zaidi Afrika Mashariki na Kati la PSSSF Commercial Complex lililopo jijini Dar es Salaam. Hatua hii itasaidia kampuni kukuza na kuongeza huduma kwa wafanyakazi na wateja kwa ujumla nchini
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi