March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waliochukua fomu Mpwapwa wapania kumtoa madarakani Simbachawene na Malima

.
Na Stephen Noel,Mpwapwa

Wanachama 17 wa chama cha mapinduzi Jimbo la Mpwapwa huku wanachama 9 wa Jimbo la kibakwe wamechukua fomu kugombea nafasi ya ubunge Katika wilaya ya Mpwapwa .

Wanachama hao waliochukua fomu Kwa majimbo yote mawili ya kibakwe na Mpwapwa ni wanachama 26 ambapo kati hao ni wanachama 4 wa kike na mmoja akiwa mahitaji maluum.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake katibu wa chama hicho Comred Denis Luhende amesema ni lazima watia nia kuzingatia kanuni na miongozo ya chama.

Aidha aliesema “kwenye zoezi la udiwani kwenye kata 33 ni wanachama 163 walijitokeza kuchukua fomu za kugombea udiwani wakiwemo wanaume 151 ambao sawa na asilimia 92 wakati wanawake ni 12 sawa na asilimia 7.9 Kwa kata zote waliochukua na kurudisha”akiongea

Hata hivyo alisema mchakato huo wa kuchukua fomu na kurudisha umefungwa rasmi hivyo mchakato unaoendelea kuwapembua ambapo Katika yote waliochukua na kurudisha fomu ni majina matatu Kila Jimbo na Kila kata ambao ndio watakao enda Katika ngazi ya kata kupigiwa kura za maoni na wanachama.

Wanachama wote walio chukua fomu hizo za kugombea ubunge na udiwani wakiwemo wabunge wote wawili wa majimbo yote mawili la kibakwe na Mpwapwa wakitetea nafasi zao akiwemo mbunge Nathan George MALIMA wa Jimbo la Mpwapwa na Mbunge George Simbachawene wa Jimbo la Kibakwe.