Na Mwandishi Wetu, TimesMajiraonline, Mufindi
WALENGWA 21 wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kati ya 34 katika Kijiji cha Isimikinyi Kata ya Malangali wilayani Mufindi, mkoani Iringa wamenufaika na mradi wa ujenzi wa barabara inayounganisha vijiji vitatu kupitia ajira za muda.
Mradi huo wa ujenzi wa barabara ulitekelezwa na wananchi baada ya kuibuliwa na Halmashauri ya Serikali ya Kijiji cha Isimikinyi, ambapo walengwa wa Mpango wa TASAF walifanyakazi na kupata malipo ya kwa kila siku kwa mwezi kwa miezi sita.
Ushiriki wa walengwa wa Mpango wa TASAF katika barabara hiyo kwa kushirikiana na jamii kumetajwa kumaliza changamoto ya mawasiliano iliyokuwepo awali katika vijiji hivyo vitatu vya Isimikinyi, Itengule na Kingege.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki msimamizi wa mradi huo upande wa TASAF, Janethkhadija Mario, amesemma mradi huo ulianza kutekelezwa Septemba mwaka jana na kukamilika Aprili, mwaka huu.
Amesema kikubwa walichokiona kwenye mradi huo ni mwitikio mkubwa wa walengwa wa TASAF, kwani wengi kwa sasa wanajua umuhimu wa kishiriki miradi inayoibuliwa ndani ya jamii.
Amefafanua kwamba fedha ambazo walikuwa wakilipwa zimewasaidia kuendeleza miradi migodo midogo ya ufugaji ndani ya familia zao na kuwajengea utamaduni wa kufanyakazi pindi fursa zinapojitokeza.
Aliongeza kuwa walengwa baada ya kuelimishwa maana ya huo mradi na faida za kushiriki kwenye kazi za ajira za muda, kaya za walengwa wa TASAF zenye watu wenye nguvu za kufanyakazi zilionesha mwitikio mzuri, na kwamba hiyo inaonesha mwanzo mzuri wa mwelekeo huo mpya wa TASAF.
Kwa mlengwa wa Mpango wa TASAF aliyeshiriki mradi huo, James Mpatule (66) mkazi ya Kijiji Isimikinyi alisema yeye na walengwa wenzake wameelimika na wameanzisha miradi ya ufugaji ng’ombe, kuku na nguruwe kupitia ruzuku ya TASAF.
Alisema kupitia elimu hiyo, pale panapojitokeza miradi ya ajira za muda ndani ya jamii walengwa wa TASAF wanajitokeza kufanyakazi ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kuimarisha miradi yao na kupata ziada kwa ajili ya kutunza familia.
Mpatule amesema elimu ambayo wamekuwa wanapata kutoka kwa wataalam wa TASAF imewawezesha kuondokana na matumizi mabaya ya fedha za ruzuku, hivyo kidogo wanachopata wanakikimbizia kwenye maendeleo..
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi