Na David John, Timesmajira Online, Mbeya
MENEJA Masoko kutoka kampuni ya kimataifa ya Mogreen inayojihusisha na usambazaji wa viwatilifu ,mabomba na ,mbolea Steven Kessy Amesema kampuni imekuwa ikijihusisha na usambazaji wa viwatilifu kwa wakulima hapa nchini hivyo wakulima wametakiwa kuendelea kutimia viwatilifu vinavyosambazwa na kampuni hiyo ilikuleta tija katika uzalishaji.
Amesema kuwa kampuniu hiyo ina bidhaa mbalimbali za kilimo ambazo wamekuwa wakisambaza kwenye madka yote yanayouza vifaa vya kilimo nakwamba wao wapo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima ili kuweza kupata tija kwenye mazao.
KESSY ameyasema haya Agosti 6 mwaka huu kwenye viwanja vya nanenane vya John Makangale Jijini Mbeya kwenye maonyesho yananenane ambayo yamebeba kauli mbiu ya ajenda 10/30 kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo ,mifugo na uvuvi.
“Katika maonyesho haya tumeleta elimu na elimu hiyo juu ya viwatilifu ambayo inatumika katika kilimo biashara, katika mazao ya Pamba ,Tumbaku,Alizeti, pamoja na Parachichi hivyo kikubwa wafike kwenye mabanda yaliyopo nanenane nakwamba tumejipanga kufungua matawi baadhi ya mikoa ili kuweza kuwafikiwa wakulima wote .”amesema Kessy
kwa upande wake Afisa kilimo wa kampuni hiyo Alex Maiko amesema kuwa kampuni hiyo ipo kwa ajili ya kumfanya mkulima aweze kunufaiki na tunatambua juhudi za serikali kupitia wizara ya kilimo katika kumpa elimu ya matumizi ya viwatilifu bora ili kuweza kumuinua kiuchumi.
“Lengo letu sisi nikuona mkulima ananufaika zaidi kwamba azalishe zaidi na kupata zaidi ili aweze kufikia kilimo biashara kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema lengo nikumfanya mkulima kunufaika.”amesema Maiko
Nakuongeza kuwa “Kulitambua hili sisi kama wadau wakilimo tunatoa viwatilifu bora na mabomba ya kumwagilizia ambayo yatamfanya mkulima kuwezzaa kuzalisha kwa tija na kupata faida kupitia kilimo.
Naye Balozi wa Kampuni hiyo Bambo amewashauri wakulima kutumia viwatilifu vinavyokana na kampuni hiyo kwani viwatilifu vyake ni bora na hakuna ubishi kwamba mkulima akitumia atapata tija nakwamba viwatilifu hivyo vinakuwa havijachakachuliwa.
Ameongeza kuwa pembejeo za kampuni hiyo ni halisi na hazina uchakachuaji wowote hivyo wakulima wajitokeze kununua viwatilifu vinatokana na kampuni ya Mogreen ambayo pia inakupa fursa ya kusafirishiwa bidhaa hiyo mara baada ya kuinunua.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best