Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online. Morogoro
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya amesema serikali imejipanga vizuri ili kuhakikisha wakulima wote nchini, wanapata mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu.
Kusaya ameyasema hayo juzi kwenye maadhimisho ya Siku ya Mbolea Kimataifa ambayo kitaifa siku hiyo iliadhimishwa katika Kitongoji cha Dakawa wilayani Mvomelo Mkoa wa Morogoro.
Katibu Mkuu huyo amesema, Wizara itaendelea kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo bora kwa wakati na kwa bei nafuu, kupitia TFRA na wadau wengine.
Amesema Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo (TARI), ipo mbioni kukamilisha zoezi la kupima sampuli za udongo katika kata zote nchini, ili kufahamu mahitaji ya virutubishi vya udongo wote kuanzia ngazi ya kata.
Kusaya amesema kwa kufanya hivyo, Wizara itakuwa na kanzi data ambayo itatoa taarifa ya upungufu wa udongo, ambapo ushauri kuhusu matumizi ya mbolea yatafanyika kisasa na kwa usahihi.
More Stories
BAKWATA yawazawadia washindi wakuhifadhi Qur’an
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya