May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakulima wa kokoa wapata ahueni malipo kwa tigo pesa

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu ya Mkononi Tigo imeanza kulipa malipo ya wakulima wa kokoa kwa njia ya tigo pesa ili kumrahisishia mkulima kupata malipo yake kwa urahisi.

Akizungumza katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kwenye maonyesho ya Nane Nane ,Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi Tigo Mkoa wa Mbeya Ronald Richard amesema,kampuni hiyo imeona njia hiyo ni rahisi kwa mkulima kupata malipo ya mauzo ya bidhaa yake badala ya kutumia njia ya Benki.

“Leo siku ya kilele cha Nane Nane sisi tigo tupo hapa katika viwanja vya John Mwakangale kutoa hamasa kwa wakulima kuhusu huduma zetu za tigo pesa kwa sababu hivi sasa tumeanza kulipa wakulima kupitia tigopesa.”amesema Ronald na kuongeza kuwa

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi Tigo Mkoa wa Mbeya Ronald Richard

“Mfano hivi sasa mkoa wa Mbeya wilaya ya Kyela tumeanza kulipa wakulima kokoa kwa njia ya Tigopesa, maana wale wakulima wa kokoa wana vyama vya ushirika kwa hiyo huwa wanakusanya kokoa yao kwa pamoja na baadaye wanauza kwa mnada kwa wafanyabiashara wakubwa.”

Aidha Ronald amesema,siku za awali walikuwa wanatumia huduma za benki ambazo pia ni nzuri lakini chanagamoto kubwa huduma za kibenki bado hazipo karibu na wateja wengi hasa ikizingatiwa wakulima wengi wanaishi maeneo ya vijijini.

“Lakini kwenye makampuni ya mawasiliano hasa tigo tuna mtandao mkubwa wa mawakala nchi nzima, kila sehemu unapoenda ni rahisi kukutana na wakala, lakini kuna huduma nyingine za kifedha kupitia benki huwezi kukutana nazo lakini ni rahisi kukutana na wakala kila unapoenda .”amesisitiza na kuongeza kuwa

“Hamasa yetu kubwa katika kilele cha siku kuu hii ya wakulima ni kuendelea kuwahamasisha wakulima wengi wanaouza mazao yao,wanafanyabiashara nyingi kutokana na vitu wanavyovizalisha kupata malipo yao kwa njia ya tigo pesa,ni huduma rahisi ni huduma rafiki inaokoa muda na gharama nyingi kama ambazo mtu labda analipwa kwa benki anahitaji kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo tofauti na wakala ambapo huwezi kutembea hatua kumi bila kukutana na wakala akakuhudumia,

“Kwa hiyo hamasa yetu kubwa ni kuwahamasisha wakulima kwamba sisi tigo tumejizatiti kuhakikisha kwamba tunawasogezea huduma nyingi kwa urahisi zaidi ili waweze kuona tija ya kile wanachokifanya kwenye shughuli zao za kilimo.” Kwa upande wake mkulima ambaye hakutaja jina lake amesema amefurahishwa na huduma ya Kamapuni ya Mawasiliano ya Tigo ya kulipa wakulima kwa njia ya Tigopesa huku akisema hatua hiyo imepunguza changamoto ya wakulima kutembea umbali mrefu kufuata huduma za benki kutokana na uchache wa huduma hiyo hasa maeneo ya vijijini.

Kwa upande wa mkulima ambaye hakutaja jina lake ameishukuru Kampuni hiyo ya mawasiliano kwa kuanza kulipa pesa zao kwa njia ya Tigo pesa huku akisema inawarahisishi kupata huduma za kifedha lakini pia kuokoa muda ambao mtu angeenda mpaka benki kwa ajili ya kutoa pesa .

“Kama mnavyojua wakulima wengi tunaishi vijijini ambako huduma za kibenki kuna maeneo ambayo hakuna kabisa hivyo humlazimu mtu hata kusafiri umbali mrefu kabisa kufuata huduma hiyo labda wilayani,kwa hiyo utaona kabisa kwa njia hii ya malipo imekuwa ni rahisi kwa mkulima kupata huduma za kifedha.”amesema mkulima huyo