Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
MHITIMU wa Chuo Cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Arusha (VETA),George Nyahende amefanikiwa kubuni mashine ya uchakataji wa matunda ambayo nisuluhusho la upotevu wa mazao na matunda kwa wakulima wengi nchini.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere,Mbunifu George Nyahinde wakati akiongea na waandishi wa habari amesema mashine hiyo ni
suluhisho ya changamoto za wakulima wengi nchini kutokana na hali waliyokuwa wanakumbana nayo kipindi cha mavuno..
Amesema wakulima wengi wamekuwa wakipata hasara kipindi cha mavuno kutokana na mazao kuwa mengi hivyo mengine kuoza hali inayofanya kupoteza mapato yao.
“Unakuta wakulima wanavuna mazao yao ambayo ni ya msimu na ukizingatia kipindi cha msimu uwa matunda yanakuwa mengi hivyo kusababisha mengine kupotea kwa kuharibika na mengine wakulima uamua kuuza kwa hasara kwa kuhofia kuharibika ,”amesema na kuongeza
“Mashine hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa fedha za wakulima zinazopotea kwa kuhakikisha wanabadilisha matunda yao na kuyachakataa kuwa ya unga na kuuza katika masoko makubwa,”amesema Nyahende.
Amesema pia mashine hii inasaidia kwa kiasi kikubwa mkulima kuuza mazao yake kwa utaratibu sio kama awali ambapo uuza kwa hasara kutokana na kuhofia kumuharibikia.
“Hii imekuwa suluhisho kwa faida kubwa baada ya kushuhudia wakulima wa vitunguu mkoani Arusha, walikuwa wakipata shida hiyo wakivuna vitunguu vyao vingine uwa vinaoza na wakija wanunuzi wanakuja na bei zao mfukoni hii inakuwa kama wanawanyonya wakulima,”amesema na kuongeza
“Wanunuzi hawaangalii gharama ya uandaaji wala nini kwani wanajipangia bei zao wenyewe,ila watakapo chakata matunda na kugeuka kuwa yaungaunga yanasaidia kuuza kwa utaratibu na kupata faida ambapo itawafanya kuwepo kwenye kilimo chao cha faida kubwa,”amesema Nyahende.
Amesema mashine hiyo inauwezo wa kukausha mazao kuanzia kilo 100 hadi tani Moja kwa wakati mmoja kulingana na ukubwa wa mashine.
More Stories
Tanzania,Uturuki kushirikiana kuinua sekta ya utalii nchini
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu