Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wakulima kutoka katika kanda ya kaskazini wanatarajiwa kupewa mafunzo maalumu kwa ajili ya kulima zao la Vanila ambalo ndilo zao la pili Linalouzwa kwa bei ghali duniani.
Mafunzo hayo ambayo yanaratibiwa na kampuni ya Vanila internationa limited Yanatarajiwa kufanyika January 28 mwaka huu Mkoani Arusha huku mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela.
Akiongea na vyombo vya habari mkurugenzi wa Kampuni ya Vanila Alisema kuwa wamemua kuleta elimu hiyo kwani zao Hilo linaweza kuwasaidia jamii kuinuka
Alisema kuwa tayari wameshafanya tafifi mbalimbali kwa mkoa wa Arusha na majibu ya tafiti hizi zimeonesha kuwa kwa mkoa wa Arusha zao Hilo linaweza kustawi kwani linastahimili.
“Takwimu zinaonesha kuwa endapo kama wakazi wa kanda hii wataweza kufanya kilimo hicho cha Vanila wataweza kupata fedha kubwa sana kwani Vanila ndio zao la pili lenye kuweza kuuzwa kwa bei kubwa Sana”aliongeza.
Aliongeza kuwa Kampuni ya VANILLA INTERNATIONAL LIMITED bado imaendelea kuwasisitiza wananchi kuwekeza katika kilimo cha vanilla kwani kilimo hicho ndicho kilimo pekee chenye uwezo mkubwa wa kukuinua kiuchumi.
Alibainisha kuwa Zao la vanilla linaloanza kuvunwa baada ya miezi 7(vikonyo) na mwaka 1 (matunda) lakini bado utahitajika kunavuna kwa miaka 60 tofauti na mazao ya Aina nyingine huku Kasi ya bei ikiwa ni kubwa Sana.
Alihitimisha kwa kusema kuwa kwa Sasa Soko kubwa la zao la Vanila lipo Dubai na sehemu nyingine duniani kwani Vanila ni moja ya mazao ambayo yanatengeneza marashi,lishe, na pia kwa mujibu wa tafiti mbalimbali pia zao Hilo likitumika ipasavyo kwa Lina weza kuimarisha afya ya ajiliNaye Meneja wa kanda kutoka katika Kampuni hiyo ya Vanila Bi Miriamu Kessy alisema kuwa hiyo ni fursa pekee kwa vijana hususani kwa vijana wa kanda ya kaskazini kwa kuwa Vanila inalipa.
Miriamu alisema kuwa uwekezaji wa zao la Vanila ni uwekezaji wa Kudumu na itaweza kunufaisha kizazi Hadi kizazi na kwa Sasa mtaji wa kuwekeza kwa zao Hilo ni wa gharama ambayo ni rafiki sana na jamii.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa