May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakinamama Mkoa wa pwani wanufaika na kilimo Cha nazi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

WAKINAMAMA mbalimbali kutoka mkoa wa pwani wamesema wamekuwa wakinufaika na kilimo cha nazi baada ya wawekezaji wengi kuwekeza katika bidhaa ya nazi na kufanya kilimo hicho kupanda thamani.


Akizungumza na mwandishi , mfanyabiashara wa kuuza na kubangua nazi, Khadija Mohamed amesema zao hilo limekuwa likipata umaarufu mkubwa kutokana na watu wengi kutumia mafuta ya nasi katika kujipakaa.


Alisema anamshukuru sana mkurugenzi wa Active Mama, Ernestina Mwenda ‘Cocunut Lady’ kutokana na kuwaunga mkono kwa kununua nazi nyingi ambazo zinawasaidia katika kujikimu katika maisha yao ya kila siku.


Alisema kampuni ya Active Mama imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia wakinamama wengi kwa kununua nazi katika maeneo yao na kufanya ubanguaji wa nazi hali ambayo inafanya inawapa ajira mara mbili.
“Kwanza tunauza nazi ambapo tumekuwa tukipata fedha za kutosha, lakini pia amekuwa akibangua nazi na kufanya tupate ajira nyingine” alisema Khadija.


Ernestina alisema amekuwa akitumia nazi za asili katika kutengeneza mafuta ya Active Mama, ikiwa kama sehemu ya kuunga mkono kilimo cha nazi lakini pia kuifanya jamii kutotumia kemikali katika miili yao.


“Unapotumia mafuta ya nazi ya asili, unafanya ngozi yako ibaki katika ubora unaostahili, lakini pia unasaidia kilimo cha nazi kwa ndani ya nchi.