Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Wakili Patrick Kipangula amesema mbali na kutekeleza majukumu ya msingi yaliyoainishwa kisheria, bodi hiyo itakuwa na wajibu wa kusimamia Mfumo wa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari nchini.
Wakili Kipangula amesema hayo leo Jumatatu tarehe 17 Machi, 2025 jijini Dar es Saalam, wakati akizungumza katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One na kuelezea majukumu ya Bodi hiyo.
Ameyataja baadhi ya majukumu kuwa ni Kutoa ithibati na vitambulisho kwa waandishi wa habari wanaokidhi vigezo vilivyoainishwa katika Sheria ya Huduma za Habari na kanuni zake, kusimamia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuzingatia maadili katika taaluma hiyo.
Wakili Kipangula amesema mbali na majukumu hayo, Bodi itaanzisha na kuusimamia Mfuko wa Mafunzo kwa Waandishi utakaokuwa na madhumuni matatu yaliyoanishwa kisheria.
Ameyataja madhumuni hayo ni kuwezesha Mafunzo kwa waandishi na wadau wa habari nchini, kusaidia au kudhamini masuala ya uandaaji wa vipindi vyenye maudhui ya ndani na kufadhili tafiti mbalimbali za kihabari na maendeleo ya Uandisi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.
Amesisitiza kuwa mfuko huo ni muhimu kwa mustakabali wa taaluma ya Uandishi wa Habari kwani kuwepo kwake ndiko kutakakofanikisha jukumu la Bodi la kuendesha mafunzo, semina, warsha na makongamano kwa Waandishi na wadau wa Habari.
More Stories
PAC yapongeza ujenzi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko Hanang’
Rais Samia ataka watakao kwamisha huduma za ardhi kuchukuliwa hatua
Kapinga : Ni maono ya Dkt.Samia wananchi wote wapate umeme