September 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakati umefika mamlaka za maji kutumia mita za Luku

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Waziri wa Maji Jumaa Aweso,ameeleza kuwa ni wakati wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza(MWAUWASA) na mamlaka za maji nchini,kuhamia kidigitali kwa kuachana na mita(dira) za maji za kawaida na kuhamia mita za maji za LUKU.

Mageuzi hayo ambayo Aweso, ameeleza yatasaidia kuondoa malalamiko kwa wananchi kuhusu kubambikiwa ankra(bili) za maji kutoka Mamlaka husika,na kuwapa fursa wananchi kutumia maji anavyotaka kulingana na kiwango cha fedha.

Aweso,ametoa kauli hiyo Septemba 8,2024, wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Buhongwa na Lwahima,katika kituo cha kusukuma maji Sahwa,kilichopo Kata ya Lwahima, jijini Mwanza,wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi huo wa maji wa dharura wenye thamani ya milioni 864.

“Nataka niwatie moyo,baada ya dhiki siyo dhiki,baada ya dhiki ni faraja,.Idara ya maji mkubali kutumia teknolojia kwa mabadiliko na mageuzi pamoja na ufanisi katiktendaji wa Wizara yetu,tukiangalia Tanesco wanatumia kita za LUKU.Ni muda muafaka,ambao ni maelekezo ya Rais Samia,mamlaka za maji nchini zinakwenda kutumia mita za LUKU za maji,”amesema Aweso na kuongeza:

“Mwananchi anataka kutumia maji ya sh 5,000, akipie,siyo siku umekaa wikiendi yako,ungepika pilau lako,Msoma Mita ng’o ng’o.Ni marufuku kumkatia mtu maji siku za mwishoni mwa Juma(weekend),Ujumla, Jumamosi, Jumapili na siku za siku kuu,”.

Pia amesema licha ya kuwa ni haki ya mwananchi kupata maji,wakumbuke wana wajibu wa kulipa ankara(bili), za maji kama inavyotakiwa.

“Ni marufuku kuwabambikia bili ya maji wananchi,kama anapaswa kulipa 10,000, akupe hiyo hiyo na siyo zaidi.Wasoma mita za maji nyumbani mnapaswa muwashirikishe wananchi pindi mnapoenda kusoma mita,ajue uniti zilizopita na sasa ili aweze kujua matumizi yake na kuepuka malalamiko yasiyo yalazima,”amesema Aweso.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, ameeleza kuwa wataendelea kubuni miradi mipya ili miradi mipya ili.kufikia maeneo mengi zaidi na kuweza kufikia asilimia 100, maeneo ya mjini ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.

Pia ameeleza kuna mradi mkubwa ambao sasa unaanza na Sahwa ni kituo kikuu,ambapo watajenga matenki makubwa matano yenye uwezo wa lita za maji milioni 31.