Na Esther Macha Timesmajira,Online,Mbeya
ILI Kuweza kukabiliana na Magonjwa yanayotokna na Mifugo wananchi wameshauriwa kushirikisha watalaamu wa mifugo kabla kufanya matumizi kwa binadamu ili kuweza kuepuka magonjwa ya yanayotokana na ulaji wa nyama ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kina madaktari wa mifugo.
Hayo yamesemwa Agosti,8 2025 na Meneja wakala ya Maabara ya Vetetinari Tanzania kituo cha Iringa (TV LA) Dkt.Geogrey Mbata wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya kilimo Nanene ambayo kikanda yamefanyika Jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale.
Amesema kuwa wameendelea kutoa elimu . kuwa ipo minyoo ambayo inaweza kuambukiza baina ya wanyama na binadamu hivyo ni vema kutafuta watalaamu ili waweze kukagua.

“Tumekuwa tukiendelea kutoa elimu kila mwaka kwa wafugaji, wazalishaji,wasambazaji wa pembejeo za mifugo na jamii kwa ujumla huwa tunakutana kwa ajili ya kuonyeshana Teknolojia na kufundishana ufugaji bora wenye tija,pia tumeonyesha aina za minyoo ambazo zinapatikana kwenye mifugo lakini ipo pia baadhi ya minyoo inaweza kuambukiza haina ya wanyama na binadamu “amesema Meneja huyo.
Hata hivyo Dkt.Mbata amesema kuwa ni vema inapotokea familia inachinja wanyama kwa shughuli yeyote ya kijamii inaweza ikawa ngazi ya kifamilia au Mtaa ni vema watalaamu wakague kwasababu kuna magonjwa ambayo binadamu anaweza kupata kupitia nyama .
Akielezea zaidi Dkt.Mbata amesema kuwa mpaka sasa wakala ya Maabara inazalisha chanjo za mifugo aina Saba ambazo ni chanjo ya kideli,homa ya mapafu kwa mbuzi,ng’ombe,na kusema chanjo zipo nyingi ambazo zinazalishwa serikali kupitia kiwanda chake ambacho kipo Kibaha.
Aidha Dkt.Mbata ametoa wito kwa wafugaji wasijikite kwenye kutafuta namna gani wanaweza kutibu magonjwa,bali watafute maarifa jinsi ya kufanya jitihada za kukinga magonjwa kabla kufika na kusema mnyama anaweza kupona Lakini anaweza vilema vya kudumu na ufanisi wake kushuka pamoja na mayai kushuka.
“Hivyo nitoe wito kwa jamii kujikita katika kukinga magonjwa kwani watalaamu wapo ngazi ya halmashauri, vijiji ,kata au kupitia wakala wa Maabara ya kanda ambao wapo Iringa na Rukwa,kwani kiasi cha asimilia 60 ya mgonjwa ambayo tunapata binadamu yanatupata yanamahusiano na Kwenye afya zetu,hivyo mifugo ambayo tunayo inaweza kuwa na faida kwetu lakini pia inaweza kuwa na changamoto kwa asilimia 60″amesema Dkt
Mbata.
Jackson Andrea ni mfugaji kutoka halmashauri ya Wilaya ya Chunya Kijiji cha Mapinduzi amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa alipata changamoto za mifugo yake kupata maradhi hivyo Kwa elimu aliyopata itakuwa msaada kwake na wafugaji wengine.
Amesema kuwa Maonesho haya ambayo serikali imekua ikiandaa kila mwaka imekuwa msaada makubwa kwa wakulima na wafugaji kujifunza vitu mbalimbali hususani kwenye eneo la mifugo.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako