January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakala wa vipimo watoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo katika Biashara

Na David John, Timesmajira Online, Mbeya

MENEJA wa Wakala wa Vipimo mkoa wa mbeya Abogasti Kajungu amesema wanashiriki kwenye maonyesho ya nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani humo nakwamba amekuja hapo ili kutoa elimu kwa wadau kuhusu matumizi sahihi ya vipimo katika biashara.

Amesema kuwa Wakala wa Vipimo ni taasisi ya serikali Ambayo dhima yake nikuhakikisha vipimo vinavyotimika katika biashara vinatumika kwa sahihi.na kauli mbiu ya maonyesho kwa mwaka huu inasema Kilimo ni biashara.

Meneja Kajungu ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye banda la Wakala lililopo kwenye maonyesho hayo ya nanenane ambapo amesema Wao wanatoa elimu kwa wakulima kuhusu ufungashaji bora

Amesema kuwa biashara ya mazao ya kilimo. Uvuvi, mifugo inatakiwa kuzimika kwa kupitia mizani iliyosahihi na kuhakikiwa na kuthibitishwa usahihi wake na Wakala wa Vipimo.

“” Tunatoa elimu kwa wakulima na wadau wengine kuhusu namna bora ya ufungashaji wa mazao ya Kilimo Kwani mazao ya Kilimo yaliyo mengi yanapimwa kwa ndoo, Visado pamoja na ndonya lakini sheria unataka mazao yote yapimwe kwenye midhani iliyohakikiwa. “amesema

Ameongeza kuwa Wakala wa vipimo kazi yake ni kuhakikisha watu wote wanafamu matakwa ya sheria .sheria ya Vipimo ya sura 340 mapitio ya mwaka 2002 Kwahiyo katika kuhakikisha mazao yanapimwa kwa usahihi wakala wa Vipimo wanahakiki mizani.


Amefafanu kuwa baada ya kuhakiki mizani wanapita kabla ya msimu kuaza wa mazao kwa mfano Pamba,Korosho wanahakiki na baadae wanafanya kaguzi za kushutukiza kuhakikisha mizani zinatumika kwa usahihi.

Ameongeza kuwa hata mizani za kwenye Uvuvi nakwenyewe wanazihakiki ili kuwa kwenye viwango vya kimataifa na hata maziwa wanayopima kwenye chupa lazima yawe kwenye Vipimo vya ujazo uliokubaliwa na kwaujumla wapo nanenane kutoa elimu na wanapata usimamizi sahihi.

“Tupo hapa ili kuhakikisha tunatoa elimu kwa Halmashauri zetu zinapata elimu sahihi kuhusu usimamizi nakutumia mizani iliyosahihi ili kumwezesha mkulima Kupata mazao sahihi kutokana na gharama anazozitumia.