May 11, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakala wa Kagere ‘azipa kisogo’ ofa

Na Mwandishi Wetu

WAKALA wa mfungaji bora mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania Meddie Kagere, Patrick Gakumba amesema bado anaendelea kupokea ofa kutoka klabu mbalimbali zinazohitaji huduma ya mshambuliaji huyo.

Licha ya kupokea ofa hizo lakini Gakumba amesema hawawezi kuzipokea wala kufanya nao mazungumzo kwani mchezaji huyo bado ana mkataba na klabu yake ya Simba unaomalizika Mei, 2021.

Wakala huyo ameweka wazi jambo hilo alipokuwa alipokuwa akihojiwa kama sababu za Kagere kutopata nafasi kunatokana na kushuka kwa kiwango chake ndani ya klabu hiyo.

Amesema, wapo baadhi ya viongozi ambao ambao wameomba
wakala huyo asaini hata nusu kataba kutokana na kutotumika ndani ya Simba lakini amewataka kuwa na subra hadi mkataba wake utakapomalizika.

“Licha ya kupokeo ofa nyingi na wengine kutaka tusaini mkataba wa awali lakini nimewaomba watulie kwani bado tunauheshimu mkataba wake ndani ya Simba uliobakiza mwaka mmoja na kwakuwa hajakiuka makubaliano na mwajiri wake mambo hayo yataanza kuzungumzwa pale mkataba wake utakapofikia kikomo, ” amesema Gakumba.

Akitolea ufafanuzi wa sababu za Kagere kutoonekana kuwa chaguo la kwanza kwa kocha, wakala huyo ameweka wazi kuwa, kukosekana kwa Kagere hakumaanishi kuwa uwezo wake umeshuka kwani uwezo wa mchezaji haufichiki hata kwa dakika chache anazoingia uwanjani.

Amesema, watu wote ikiwemo viongozi na mashabiki wanajua uwezo wake hivyo kikubwa kwa sasa ni kuendelea kuwa na subra kwani bado mechi zipo nyingi na anaimani kile alichokifanya misimu miwili iliyopita ataendelea kukifanya msimu na muda utaongea.

“Ninaiheshimu sana Simba kwani ni timu nzuri na nimefanya nao kazi vizuri na hadi sasa wnaendelea kutimiza yale yote yaliyo ndani ya mkataba na mchezaji wangu. Mambo ya kutopangwa si ya uongozi bali ni ya benchi la ufundi hivyo watu waendelee kusubiri kwani muda utaongea,” amesema Gakumba.