Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar
KATIKA kuelekea siku ya Kimataifa ya mtoto wa kike Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 11 Shirika la Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAJIKI) limesema ni jukumu la kila mmoja kumlinda mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto zake.
Akizungumza Jijini Dar es salaam katika mkutano uliowakutanisha wakazi wa Makumbusho pamoja na wadau mbalimbali, Mkurungezi wa WAJIKI ,Janeth Mawinza amesema mtoto wa kike amekuwa akikumbana na chagamoto nyingi katika jamii inayomzunguka jambo ambalo limekuwa likisababisha kushidwa kutumiza malengo yake.
Amesema mama huanzia katika usichana na badae kuwa mama na kiongozi bora hivyo wakilindwa na kupata malezi na ushirikiano itasaidia zaidi kupunguza chagamoto na hatimaye kupata viongozi bora .
Mawinza amesema katika kukabiliana chagamoto hizo WAJIKI kwa kushirikiana na Kituo cha Taarifa na Maarifa Makumbusho wamefanikiwa kuibua matukio ya ukatili kwa watoto wa kike na wanawake katika maeneo hayo.
“Katika Kutekeleza miradi yetu ikiwemo kampeni ya safiri salama bila rushwa ya ngono inayoendeshwa chini ya ufadhili wa Women Tanzania Trust Fund tumefanikiwa kuibua matukio ya ukatili kwa watoto wa kike na wanawake huku kesi mbalimbali zikiibuliwa.
“Kampeni hii huendeshwa kwa kuwapa nafasi watuhumiwa kupata elimu wakimemo madereva daladala pamoja na madereva bodaboda kutambua umuhimu wa kuwalinda waoto wa kike na mwanamke na dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono”amesema.
Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuvunja ukimya pamoja na kuhakikisha popote mtoto wa kike na mwanamke wanapopita wanaume wanapaswa kuhakikisha anakuwa salama.
Wakizungumza katika mkutano huo baadhi ya wazazi wamelipongeza shirika hilo na kulitaka kuendelea kutoa elimu zaidi kwani jamii bado aina uelewa wa kutosha.
Warda Nasoro ni mmoja wa Wazazi walioshiriki katika mkutano alisema baadhi ya Wazazi wamekuwa wakichangia kuwepo kwa vitendo vya rushwa ngono kutokana na kutokuwafatilia kila hatua ya watoto wao .
Amesema rushwa ya ngono sio tu hufanyika barabarani au katika vyombo vya moto ameeleza kuwa hata majumbani hufanyika pia.
Nasoro Omary ni mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Makumbusho amebainisha kuwa wazazi wengi wamekuwa bize sana jambo ambalo uchangiaji kwa kiasi kikubwa mtoto wa kike kujiingiza katika vitendo vya rushwa ya ngono bila ya kujua kwani anakuwa na Uhuru wa kufanya jambo lolote pasipo uangalizi wa walezi wake.
“Wazazi wengi wanachangia kuwepo kwa vitendo hivi unakuta mzazi ni mkali sana au yuko bize sana hivyo tunaomba Wazazi wetu kuwa karibu na sisi kwani kwa pamoja tunaweza kusaidia kupunguza na Kupambana na vitendo vya rushwa ya ngono”amesema .
Kwa upande wake Dereva wa Daladala Issa Hamad amesema amewahi kushuhudia vitendo vya ukatili wa kigono kwa wanafunzi huku watuhumiwa zaidi wakiwa wanaume .
Amesema wanafunzi wamekuwa Wahanga wakubwa kwa ukatili wa kigono pale wanapokuwa wanasubir usafir kwa ajili ya kurudi nyumbani au kwenda shuleni.
“Nimewahi kumuona mbaba akiandika namba yake ya simu katika karatasi pindi anapomuona mwanafunzi kakosa siti umpatia shilingi elfu 10 pamoja na karatasi hiyo “amesema Hamad.
Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Kinondoni Zena Nalipa amesema Serikali imekuwa katika mapambano dhidi ukatili wa kijinsia hivyo aliiasa jamii kutokufumbia macho vitendo hivyo ambayo upelekea mtoto wa kike na mwanamke kutokufikia malengo yake.
Mbali na utoaji elimu juu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa kigono kwa watoto wa kike wanawake pia WAJIKI ilitoa elimu juu ya Kupambana na Ugonjwa wa UVIKO 19 na kuitaka jamii kuchukua tahadhari sambamba na kwenda kupata chanjo .
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu