November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wajasiriamali watakiwa kutumia fursa AFCFTA

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Wajasiriamali na watanzania kwa ujumla wametakiwa kutumia ipasavyo fursa mbalimbali zinazotokana na uwepo wa soko huru la biashara afrika (AFCfTA) katika kutanua wigo wa usambazaji wa bidhaa wanazozizalisha hali itakayosaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa taifa na wa bara la afrika kwa ujumla

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na mwakilishi wa waziri wa viwanda na biashara kutoka nchini Ghana Koffi Addo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wafanyabiashara kutoka Ghana ambapo pia amesisitiza waafrika kufanya biashara wao kwa wao kwani bara hilo lina idadi kubwa ya watu hali inayotoa fursa ya kuchagiza ukuaji wa biashara za ndani

Kwa upande kwake meneja usimamizi na ukuzaji biashara kutoka Tantrade Mohammed Tajari alisema maonyesho hayo yatatoa fursa kwa wafanyabiashara nchini kubadilishana uzoefu na wafanyabiashara kutoka nchini ghana pamoja na kuwezesha unafuu wa kodi baina ya nchi zilizopo katika soko huru la AFCfTA

“maonyesho haya ya Ghana Expo tumepata fursa kwa wafanyabiashara mbalimbali ambapo wameweza kubadilishana mawazo na biashara na vilevile kujenga muktadha wa bidhaa tulizokuwa tunazikosa Tanzania na wao pia walizikokuwa wakizikosa Ghana” alisema Tajiri.

Naye mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara wanawake Tanzania Mercy Sila alisisitiza kuwa maonyesho hayo ni muendelezo wa kuboresha soko huru la Afrika na kubainisha kuwa zaidi ya makampuni 70 kutoka nchini Ghana yameshiriki maonyesho hayo

“Hapa tumekutana nchi mbli za kiafrika tukiendeleza mpango mzima wa soko huru la Afrika, wenzetu wamekuja makampuni 70ya wafanyabiashara ambapo wameleta bidhaaa ambazo kwa kiasi kikubwa sisi tunazihitaji na wao pia wameona zile wanazozihitaji kutoka kwetu hivyo tunaona ni kitu ambacho kitaleta manufaa” alisisitiza Mercy.

Nao baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo wabainisha kuwa yatasaidia katika kubadilishana uzoefu baina ya wafanyabiashara wa bara hilo na hivyo kuongeza ubora wa bidhaa na hatimaye kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa pamoja wa bara hilo