Na Heri Shaaban, Timesmajira Online -Kivule
Mwanasheria Anita Waitara mtiania nafasi ya Ubunge,ambaye ni mmoja ni miongoni mwa watakaopigiwa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM),ameahidi kuboresha miundombinu ndani ya Jimbo la Kivule,endapo atapata ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka huu
Akizungumza wakati wa kuomba kura za maoni ndani ya CCM Kata ya Majohe jimboni Kivule,Waitara, amesema, atabadirisha jimbo hilo liwe la kisasa kwa kuleta maendeleo katika huduma za jamii.
“Kwa taaluma mimi ni Mkemia pia Mwanasheria, miaka 30 sasa naishi kwenye Jimbo hili,na changamoto za Kata ya Majohe nazifahamu ikiwemo miundombinu ya barabara, hivyo mkinichagua nitashirikiana na Serikali kuboresha miundombinu yote ikiwemo ya sekta ya afya,elimu ikiwa ni pamoja na kujenga shule za mchepuo wa kiingereza pamoja na kuongeza vifaa tiba,”.
Pia amesema,tashirikiana na Serikali kutafuta wafadhili pamoja na kusimamia mazingira kwa kuleta magari ya kubeba takataka kwa kila Kata ili mji wa Majohe na Jimbo hilo liweze kuwa safi.
Aidha atachimba visima ili aweze kumtua mama ndoo kichwani sambamba nakuleta bima ya afya kwa wazee kwa ajili ya matibabu na kushirikiana na taasisi zote za dini pamoja na kuwainganisha vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi.
” Mimi ni mwanamke nitasimama na wanawake wezangu katika mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri,ili waache kukopa kausha damu sambamba na kuunda vikundi vya wanawake na bodaboda,”.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi