January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waipongeza Serikali miradi ya zaidi ya tirioni moja

Na Ashura Jumapili, TimesMajira online Kagera

Vikundi mbalimbali vya Wananchi kikiwemo kikundi cha Kagera Mpya Bendera Mbili,mkoani Kagera wameipongeza Serikali kwa kuwaletea miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya tirioni moja.

Huku wakitengeneza bango maalumu la shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Hajath Fatima Mwassa,ambalo wameliweka katika eneo la makutano ya barabara ya Biharamulo na Uganda, lenye ujumbe unaosomeka,”Asante RAis Samia kwa miradi uliyotuletea Kagera,juhudi zako tunaziona,Asante mama kutuletea mama anatufaa”.

.

Hashim Haruna mkazi wa mtaa wa Miembeni Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba,amesema katika Mkoa huo,wamekuja viongozi mbalimbali walio kuwa wakisimamia maendeleo ya Wananchi lakini hawakuweza kuonesha ushirikiano wenye tija katika maendeleo kama yaliyofanyika kwa kipindi hiki.

“Mkoa umekuwa ukipokea viongozi mbalimbali ambao walitakiwa wasimamie maendeleo, lakini hawakuweza kufikia viwango vinavyo wasaidia Wananchi katika kuonesha mianya ya uchumi na maenedeleo kama, makongamano ya kumbusha wazawa kuendeleza uchumi wa Mkoa wao na kudumisha mila na desturi zetu,”anasema Haruna

Anath Rwabukoba mkazi wa Kata ya Rwamishenye,amesema maendeleo ya watu yanafanywa na viongozi walioaminiwa kuwasaidia Wananchi katika kuwavusha kwa mambo mbalimbali ya jamii,ikiwemo kujikwamua kiuchumi na kuwajengea miundombinu mbalimbali kama vile barabara,sekta ya afya,elimu,kilimo na uvuvi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajath Fatuma Mwassa,amesema mafanikio na maendeleo ya Mkoa huo kwa sasa yametokana na ushirikiano ambao aliutengeneza tangu awali kwa nguvu kuhakikisha wanakuwa wa moja.

Hajath Mwassa,amesema alipofika mkoani Kagera, kwanza aliwaunganisha wanakagera wote kuwa wa moja,kupendana ,kuheshimiana,mshikamano na wasigawanyike vipande vipande au vikundi.

“Kwa namna yoyote tusingekuwa na umoja na mshikamano leo hii tusingekuwa wa kwanza kitaifa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024,likifanyika jambo Mkoa wa Kagera unatazamwa kwenye nafasi ya 5 na siyo mkiani kama ilivyokuwa awali kutokana na mshikamano uliopo kwa wananchi na viongozi wa serikali,”amesema Hajath Mwassa.

Awali katika hafla hiyo ya pongezi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,alipiga simu na kuwapongeza wananchi kwa kuonesha mfano mzuri wa kumpongeza Rais kwa majukumu anayoyafanya .

“Nimefurahi sana kusikia wananchi wanampongeza Rais kwa kazi nzuri anayofanya na kuwaletea kiongozi makini wa kusimamia maendeleo ya Mkoa wao,”amesema Majaliwa.

Hata hivyo amempongeza Justine Kimodoi anayeishi nje ya nchi kwa ubunifu wake wa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.