Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM
WAHITIMU wa chuo cha Amana Vijana Centre Mkoani Dar es Salaam watakiwa kutumia taaluma zao katika kuziendea fursa mbalimbali za ajira.
Hayo yameelezwa jijini na Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam Adam Paulo katika mahafali ya 21 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliopo Ilala ambapo jumla ya vijana 158 walihitimu kozi mbalimbali.
”Taaluma mlizozipata hapa chuoni zitumieni kama ngao ya kuelekea kwenye mafanikio huko muendako msikubali kubweteka, ”amesema Paulo
Aidha Paulo amesema miongoni mwa changamoto alizozisikia atazifanyia kazi ikiwemo la uhaba wa vyumba vya kujisomea na vifaa vya kujifunzia kwa kukutana na wadau wake.
Hata hivyo katibu huyo amewasihi vijana kuzingatia nidhamu katika kuziendea fursa za ajira akiwemo kujiajiri wao wenyewe.
Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo hicho Phillipo Ndokeji amewataka wahitimu kutobweteka ila wajizatiti na taaluma walizozipata chuoni hapo.
Mkuu huyo amewasihi wazazi kuwa macho na vijana wao kipindi ambacho wamemaliza mafunzo yao.
Nae mhitimu wa kozi ya hoteli aitwae Abdallah ameeleza ujuzi alioupata hapo chuoni itakuwa ni kigezo cha jitihada sehemu anayotegemea kuanza kazi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa