Na Rose Itono,Timesmajira
WAHITIMU waliosoma Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) wametakiwa kutumia midahalo mbalimbali kwa kutoa maoni yatakayokiendeleza chuo na taifa kwa ujumla
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho kwenye kusanyiko la wahitimu waliosoma MNMA Dar es Salaam jana Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma MNMA Prof. Richard Kangalawe amewataka washiriki wa kusanyiko la mwaka 2024 kutoa maoni yatakayokiendeleza chuo
Amesema kusanyiko la wahitimu lilianzishwa rasmi Oktoba 2010 wakati wa mahafali ya tano ya chuo ili kukutanisha hazina kubwa ya waliohitimu hapa ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa hili.
Amewataka kuendelea kutumia makusanyiko hayo kwa kutoa maoni kwa njia ya midahalo mbalimbali yenye nia
ya kuendeleza chuo na uzalendo kwa taifa.
Aidha amesema kupitia mapendelezo yanayotolewa na kusanyiko hili chuo kimeweza kufanya maboresho mengi kuhusu mustakabali wake
Amewasihi kujadili vema mada Kuu katika kusanyiko la mwaka huu ambayo inasema ‘Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kinavyojipambanua katika kuchangiza Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii’
Pia amesema chuo kimepokea changamoto mbalimbali zinazokabili shughuli za utekekezaji wa majukumu ya kusanyiko ikiwepo kutokuwa na ofisi inayojishughulisha kipekee na shughuli hizo na kuahidi chuo kitaanzisha ofisi maalumu kwa ajili ya kushughulikia shughuli za kusanyiko
Amefafanua historia ya chuo hicho Prof. Kangalawe alisema Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kina historia ndefu na kwamba lilianzishwa Julai 29 1961, na kina historia ya kuwa kitovu Cha kufundisha maadili kwa viongozi wa umma.
Amesema dira ya chuo ni kuwa kitovu Cha utoaji wa maarifa bora kwa kutoa elimu
na mafunzo kuhusu ubunifu na uvumbuzi na kuendeleza amani na Umoja wa kitaifa
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19