WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Ikulu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar CPA Jamaal Kasim Ally, amewaagiza wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini kufanya kazi kwa kuendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia ili kuharakisha utoaji wa taarifa za mahesabu kwa umma.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA), ambapo amewataka wahasibu kushirikiana na serikali mtandao ili kuendana kasi teknolojia ya habari na mawasiliano.
Hata hivyo amewasihi wahasibu na wakaguzi kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia miiko na maadili ya kazi yao kwani taaluma hiyo ni muhimu katika uchumi wa nchi na ustawi wa maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania Prof. Sylivia Temu amesema bodi hiyo imejipanga kwa miaka miwili ijayo kuanza kutoa taarifa za uendelevu wa taasisi za umma na binafsi itakayoonyesha faida na athari zake kwa jamii.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito