NA
K-VIS BLOG, UDSM
BIASHARA
ya Kaboni ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi duniani, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano Bw. Abdallah
Hassan Mitawi amesema.
Bw.
Mitawi ameyasema hayo katika warsha ya kuwajengea uelewa wa Kanuni na Mwongozo
wa biashara ya kaboni kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini Juni 19, 2023
kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), sehemu ya Mlimani.
Alisema
biashara hiyo hufanyika miongoni mwa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya
Tabianchi, Itifaki ya Kyoto na Makubaliano ya Paris.
“Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ni nchi Mwanachama wa Mikataba hii. hivyo, pamoja na
sera na mikakati iliyopo na kwa kuzingatia umuhimu wa biashara hii, Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa Kanuni na Mwongozo wa Taifa wa
Usimamizi wa Biashara ya Kaboni nchini.” Alifafanua Bw. Mitawi.
Akizungumzia
Malengo makuu ya Kanuni na Mwongozo huu alisema, nipamoja na kuweka utaratibu na masharti
ambayo wadau na wawekezaji wa biashara ya kaboni watapaswa kuzingatia wakati wa
utekelezaji wa miradi mipya na miradi inayoendelea ya biashara ya kaboni katika
sehemu mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kanuni
na Mwongozo zilishatangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 636 la tarehe 28
Oktoba, 2002. hivyo, kuwa tayari kwa matumizi.” Alibainisha.
Nyenzo
hizi zimejikita katika kuimarisha mchango wa nchi katika jitihada za kupunguza
uzalishaji wa gesijoto na hivyo kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa
kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa ajili ya maendeleo endelevu, alisema.
“Mtakubaliana
nasi kuwa sote kwa pamoja tunapaswa kuchukua hatua mahususi ili kuimarisha
hifadhi ya mazingira nchini kwa maendeleo endelevu, hivyo basi, kupitia warsha
hii ni matumaini yetu kuwa sote kwa
pamoja kupitia taasisi zetu tutashirikina katika kusimamia utekelezaji wa
Kanuni na Mwongozo wa biashara ya kaboni nchini ikiwa ni pamoja na kutoa
taarifa sahihi.” Alisisitiza Bw. Mitawi.
Tayari
Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) imesaini makubaliano ya awali
(MoU) ya kufanya biashara ya Hewa Ukaa (Carbon dioxide -CO2) na Kampuni ya
Kigeni ya GreenCop Development PTE LTD Mei 18, 2023 jijini Dar es Salaam.
Awali Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda alisema kuna makampuni mengi yameleta maombi ya kuwekeza kwenye eneo hili, na matatu yako kwenye hatua za mwisho.
“Kampuni
ya GreenCop PET Ltd inahusisha maeneo matatu ambayo ni pori la Akiba la Selous,
Kilombero na Msanjesi.
Baadhi ya washiriki
Bw. Abdallah Hassan Mitawi
Baadhi ya washiriki
Mgeni rasmi na washiriki
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa