October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahamiaji haramu 36 wakamatwa Dar,Kunege atoa onyo

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Dar

NYOMBO vya ulinzi na usalama Mkoa wa Dar es Salaam vimefanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji haramu 36 ambao ni raia wa Ethiopia na Somalia walioingia nchini kinyume na taratibu.

BOFYA HAPO JUU KUANGALIA LIVE MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa huo Aboubakar Kunenge ametoa onyo kali kwa raia wa Tanzania wanaoshiriki kuwafadhili na kuwasafirisha ili wapate fedha.

RC Kunenge amesema wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia November 15 kwenye fukwe za Mbweni ambapo kati yao 30 wanatoka nchini Ethiopia na sita wanatokea nchini Somalia.

Wahamiaji haramu waliokamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha RC Kunenge amesema hata utaratibu unaotumika kusafirisha watu hao unakiuka sheria,haki na utu wa binadamu sababu wengi wao wanafungiwa kwenye kontena zisizokuwa na hewa na pindi wanapobainika kufariki maiti zao hutupwa kwenye vichaka.

Pamoja na hayo RC Kunenge amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.

Afisa uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Kamishina Msaidizi Edmund Mrosso amesema wahamiaji hao watafikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini kinyume na taratibu.

Aidha Kamishina Mroso amesema kwa wale wanaowasafirisha au kuwahifadhi wahamihaji hao adhabu inaelekeza kifungo cha miaka 20, faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizotumika.