Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Rai 14 wa nchini Burundi,wamekamatwa na Jeshi la mkoani Mwanza, kwa tuhuma za kuingia nchini hapa kinyume na Sheria kwa kutumia usafiri wa magari mawili tofauti ya abiria.
Akizungumza na umma kupitia vyombo vya habari wilayani Sengerema mkoani hapa, Novemba 23,2025,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP.Wilbrod Mutafungwa,alisema,kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na ufuatiliaji wa mienendo ya kihalifu na uwekaji wa vizuizi barabarani,katika Kijiji cha Busisi, Tarafa ya Sengerema.
DCP.Mutafungwa, alisema kati ya wahamiaji haramu hao 13 walikamatwa Novemba 23,2025 majira ya saa 7:30 mchana,wakiwa wanasafiri ndani ya gari aina ya Tata yenye usajiri T. 337 DYA, mali ya Chiza Francis Lugubi, mkazi wa Dodoma, linalofanya safari zake kati ya Kabanga (Ngara, Kagera) na Mwanza.
Kwa mujibu wa DCP.Mutafungwa,alisema wakati wa kukamatwa, dereva wa gari hilo, aliyetambulika kwa jina la Jonas Richard, alifanikiwa kutoroka eneo la tukio na jitihada za kumsaka zinaendelea.
Pia amesema,watuhumiwa wengine waliohusika katika usafirishaji walikamatwa ambao ni Mustahper Emily(24),fundi magari, na mkazi wa Kahama, Shinyanga na
Pendo Matembere(36),kondakta na mkazi wa Nyegezi Mwanza.
Baada ya kuhojiwa, ilibainika kuwa wahamiaji hao waliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga, mkoani Kagera, mnamo Novemba 22,2025.
Huku mtuhumiwa wa 14, Shadia Majaliwa(18), raia wa Burundi na mkazi wa Kisuru, alikamatwa eneo la Nyatukara wilayani Sengerema akiwa ndani ya gari aina ya Yutong lenye namba za usajili T 131 DRE.
Magari yote mawili yamekamatwa na dereva pamoja na wasaidizi wengine wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuwasafirisha wahamiaji haramu.
Aliwataja wahamiaji haramu hao kutoka nchini Burundi kuwa ni Nkurunzinza Eloi,Bizimana Aster,Tanishaga Renova,Nyosaba Anatory, Niyokuru Jlock, Nsolimana Evariste na Riyazimana Jerome.
Wengine ni Mbonipa Claude,Ntirampera Oleste,Mbalishimana Swalidi,Sindobizero Oscar,Irakize Derise,Elias Sinilemeya, miaka 31 na Shadia Jafari.
Sanjari na hayo Mutafungwa alisema litaendelea kuimarisha doria na vizuizi vya barabarani kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na wananchi ili kudhibiti matukio ya kihalifu.
Aidha,aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwafichua wahalifu popote walipo, ili waweze kudhibitiwa kabla hawajafanya uhalifu wowote.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi