November 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wagombea 1798,kushiriki uchaguzi Serikali za Mitaa

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Jumla ya wagombea 1798, kutoka vyama 15 vya siasa watashiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27,2024, katika mitaa 171 ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Ambapo uteuzi wa wagombea hao ulifanyika Novemba 8,2024.

Wagombea hao wanatoka katika vyama vya siasa mbalimbali ikiwemo Chama Cha Mapinduzi(CCM), CHADEMA,ACT-Wazalendo,SAU,UMD,CUF,UPDP,NCCR,CCK,DP,UDP,AAFP, Demokrasia Makini,ADC na NLD.

Hayo yameelezwa Novemba 17,2024 na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Ummy Wayayu,wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wilayani Ilemela.Ambapo amesema kati ya wagombea hao 373, ni walioteuliwa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Serikali za Mitaa.

Kati yao katika nafasi ya Uenyekiti kutoka CCM ni 171, CHADEMA 113, ACT-Wazalendo 32,SAU 9,UMD 4,CUF 4,UPDP 7,NCCR 3,CCK 10,DP 7,UD1q1a atP 2,AAFP 4, Demokrasia Makini 9,ADC 2 na NLD 6.

Huku 1425, ni wagombea walioteuliwa kugombea nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Mtaa kundi mchanganyiko na kundi la wanawake,kati yao kutoka CCM ni 855, CHADEMA 537,ACT-Wazalendo 16,SAU 0,UMD 0,CUF 8,UPDP 0,NCCR 0,CCK 0,DP 0,UDP 5,AAFP 0, Demokrasia Makini 0,ADC 4 na NLD 0.

“Wagombea wote walichukua na kurudisha fomu,waliteuliwa isipokuwa wanne waliomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa, kwa Mitaa ya PPF Kata ya Kiseke,Iseni Kata ya Kayenze,Kangaye ‘A’ na Kangaye ‘B’ Kata ya Nyakato,hawakuteuliwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiandikisha kupiga kura kwenye kituo zaidi ya kimoja,kutojiandikisha katika orodha ya wapiga kura pamoja na kutotumiza umri wa miaka 21 unaotakiwa kisheria ili mtu aruhusiwe kugombea,”amesema Wayayu.

Amesema,uwasilishaji wa pingamizi ulikuwa 8-9,Novemba,2024, hadi mwishoni wa upokeaji wa pingamizi Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilipokea jumla ya pingamizi 144,zilizohusiana na kuteuliwa,kati ya hizo pingamizi 75, zilihusiana na kupinga uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa na 69, zilihusu wagombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya mtaa.

“Pingamizi moja lilihusiana na kutoteuliwa kwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa.Kufuatia mapingamizi hayo jumla ya wagombea 17 wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa waliokuwa wameteuliwa hapo awali, uteuzi wao ulitenguliwa na kwa upande wa wagombea wa ujumbe wa Kamati ya mtaa walioenguliwa ni 3,” amesema Wayayu na kuongeza:

“Wagombea waliokata rufaa kwenda Kamati ya Rufaa ni 20, na baada ya kusikiliza rufaa hizo Kamati hiyo ilifanya uamuzi wa kuwarejesha wagombea watatu ambapo wawili ni nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa katika mitaa ya Nyanda Kata ya Nyasaka na Kilimahewa ‘B’ , Kata ya Nyamanoro na mmoja ni mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya mtaa wa Nyagungulu Kata ya Ilemela,”.

Hata hivyo amesema,zoezi la uchukuaji fomu na urejeshaji likianza Oktoba 26,2024 hadi Novemba 1,2024, ambapo jumla ya wagombea 414 wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa kutoka vyama mbalimbali wakijitokeza.Jumla ya mitaa 34 kati ya 171 wagombea waliomba nafasi hiyo walikuwa kutoka CCM pekee.Hivyo baada ya Kamati ya Rufani kuwa imekamilisha kazi yake mitaa 48 itakuwa na wagombea wa CCM pekee ambao watapigiwa kura za ndiyo au hapana.

Sanjari na hayo amesema, Halmashauri hiyo inatarajia kuwa na jumla ya vituo vya kupiga kura 493 katika uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Novemba 27,mwaka huu.Huku akitumia fursa hiyo kuhimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua viongozi wanaowataka.

“Oktoba 11 hadi 0ktoba 20,mwaka huu kulikuwa na zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura ambapo lengo lilikuwa kuandikisha watu 302,329 wanaume ni 139,665 na wanawake 162,664.Lakini hadi kufikia Oktoba 20,2024 Halmashauri iliweza kuandikisha watu 297,230 kati yao wanaume 148,936 na wanawake 148,294 sawa na asilimia 98.3 ya lengo,”.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha DP Wilaya ya Ilemela,Rebeka Mwita,amesema toka mwanzo wa mchakato wa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa vyama vyote wamekuwa walishirikishwa kil

“Ndani ya chama chetu uteuzi ulifanyika kwa uwazi,hakukuwa na rushwa ya ngono kwa wanawake,walihamasishwa walijitokeza kwa wingi na kupata nafasi za kuwakilisha chama kwenye uchaguzi huu wa Serikali ya Mtaa,”.

Katibu wa chama cha Demokrasia Makini Wilaya ya Ilemela,Mohamed Msanya,amesema tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi hawajaona dosari yoyote mpaka sasa kwa asilimia 80 kuelekea 90, wagombea wamepata haki yao.

“Hatujaona dosari kwani tumeshirikishwa tangu mwanzo wa mchakato na kila hatua,baada ya uchaguzi maisha mengine yanaendelea vile vyama ambavyo vinaashiria uvunjivu wa amani sheria zipo,waache watu wafanye uchaguzi kwa amani, ili wananchi wapate fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka.Pia watakaoshindwa wawaunge mkono watakaoshinda,”.