Na Penina Malundo,Times Majira Online, Dar es Salaam
WAFUGAJI, Ng’ombe wa maziwa wilaya ya Kinondoni, wameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini pamoja na Bodi ya Maziwa kuwasaidia kuwakopesha mashine za usindikaji maziwa.
Ombi hilo lilitolewa leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba na Mwenyekiti wa Ushirika wa Wafugaji hao, Kajia Mrita.
Akitoa ombi hilo Mrita amesema, hali ya uzalishaji wa maziwa katika wilaya yao ipo juu ukilinganisha na miaka ya nyuma hivyo uongezwaji wa thamani na usindikaji wa maziwa utaweza kuwafanya kuuza maziwa kwa bei nzuri kuliko sasa.
“Tutakapo saidiwa mashine hizi na serikali tunaamini kwa kiasi kikubwa tutasindika maziwa haya, na kuyafanya kuwa na bei nzuri zaidi kuliko vile tunapokamua na kuuza moja kwa moja,”amesema na kuongeza.
“Mashine hizo zilizopo katika maonesho hayo yenye ujazo wa lita 200 hadi 500 endapo tutapata mashine hizi tunaamini soko la maziwa litazidi kuongezeka,”amesema.
Amesema, ni vyema serikali ingewasaidia kupata mashine hizo ili ziweze kuwasaidia katika ufugaji wao.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja