Na Rose Itono,Timesmajira
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa leo amewatunuku vyeti na kuwakabidhi zawadi ya Fedha taslimu watumishi 20 ambao wameshinda nafasi na kuwa Wafanyakazi bora katika mwaka wa fedha 2024/2025
Wafanyakazi hao ni kutoka katika Kurugenzi, Idara na Vitengo kwa kampasi zote za Chuo hicho .
Akizungumza na Menejimenti na Wafanyakazi hao Prof.Mapesa amewapongeza kwa ushindi huo na amewataka Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidi, nidhamu na Uzalendo ili kufikia Malengo ya Taasisi na Taifa kwa ujumla.
Prof. Mapesa amesema teknolojia inazidi kukua hivyo amewataka Watumishi kuona namna bora ya kutumia E- Learning, na kuona ni namna gani vifaa na mifumo ya Kisasa viitaweza kutumika ili kuwafikia wadau wengi .

Prof. Mapesa amesema ni wajibu wa kila Mtumishi kufanya mahala pa kazi kuwa mahala pa furaha, Amani, na sehemu salama kwa kuwa muda mwingi mtumishi anatumia muda wake akiwa kazini.
Aidha amewasisitiza Wanataaluma kuhakikisha wanafanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu
“Jipangeni kuandika na kuchapisha ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wateja (Customer care), kujali wateja ni jambo la msingi sana,”amesisitiza Profesa Mapesa.

Katika hatua nyingine Prof. Mapesa ameungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuomboleza kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya ambapo amesema Taifa limepoteza mtu muhimu kwa namna moja ama nyingine kwa kuwa Mzee Msuya alikuwa ni miongoni mwa Wazee walioshirikiana na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kukijenga Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Mipango, Fedha na Utawala Dkt. Evaristo Haulle alivitaja vigezo vilivyotumika kumpata Mfanyakazi bora kuwa ni sharti awe Mtumishi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa muda usiopungua mwaka mmoja, awe na mahusiano mazuri na viongozi na Wafanyakazi wenzake, asiwe mtu wa Majungu na awe tayari kulinda Uchumi na kudumisha Amani.
Katika hafla hiyo ambayo ilishirikisha viongozi wa vyama vya Wafanyakazi, Chama cha Wafanyakazi wa Taaasisi, Elimu ya juu, Sayasni, Teknolojia, Ufundi Stadi, Habari na Utafiti (RAAWU), Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) na MNIMASA.
Kwa upande wa Wafanyakazi bora waliowakilisha Chuo Dkt. Willy Maliganya upande wa Wanataaluma, na Bwana. Atanas Limbu upande wa Waendeshaji wameushukuru Uongozi wa Chuo na kusema kuwa zawadi zilizotolewa zinatoa motisha kwa Wafanyakazi kujituma na kufanya vizuri na kuwa ushindi uliopatikana siyo wa kwao peke yao bali ni wa Chuo kizima.
More Stories
Madiwani Ilala walia na dampo la Pugu
TLS yaishauri serikali kuanzisha chombo maalumu
Ridhiwani ataka watu wenye ulemavu wapewe fursa