Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WIZARA ya habari, mawasiliano na Teknolojia ya habari imekutana na wafanyabiashara mbalimbali wa Jiji la Dodoma kuwapa mafunzo kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi utakaosaidia kuinua uchumi kidigitali
Akizungumza katika mafunzo hayo jijini hapa leo,Desemba 13,2022,Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Dodoma Aloyce Mogofi amesema kikao kazi hicho ni muhimu kwa kuwa kinalenga kujenga uelewa wa pamoja katika kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi.
Ameeleza kuwa kwasasa mfanyabiashara ili afanyebiashara yake kwaufanisi na kukuza kipato kwaharaka ni vyema akatumia mfumo wa anuani za makazi.
“Ukitumia anuani ya makazi ni rahisi kumuelekeza mtu akakupata kwa haraka kwasababu atajua mtaa wako lakini pia atajua namba ya nyumba unayokaa itakurahisishia wewe kama mfanyabiashara kufikiwa bila shida na wateja wako,”amesema Mogofi.
Mogofi amesema kuwa kundi hilo la wafanyabiashara limeonekana ni muhimu hivyo linapaswa kupewa maelezo,ujuzi,taarifa muhimu Kwa ajili ya kufanikiwa kibiashara.
“Lazima tuelewe kuwa maendeleo ya biashara yanayegemea zaidi mfanyabiashara anayejitambua na kukubali kwenda na wakati,”amesema
Kwaupande wake Mtaalamu wa Tehama, Wizara ya ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi Anord Mkude,akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi kwenye mafunzo hayo amesema umuhimu wa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini ni kuwezesha mipango na tafiti kufanyika kwa tija, kuongeza vyanzo vya fedha , kuimarisha usalama ,kuwezesha utoaji , upatikanaji na upelekaji wa huduma za bidhaa hadi mahali husika.
Mkude ametaja manufaa mengine kuwa ni kusaidia wawekezaji kufanya maamuzi kabla ya kuamua kufanya uwekezaji na kuwezesha biashara mtandao kufanikiwa hali itakayo inua fursa ya uchumi wa kidigitali.
Pamoja na hayo Mkude ameeleza muundo wa anwani za makazi kwa upande wa vijijini kuwa unahusisha namba ya nyumba au jengo,jengo la kitongoji au shehia na namba maalumu ya postikodi na kwa upande wa Miji,muundo wa anwani za makazi unahusisha namba ya nyumba ,jina la mtaa au barabara,namba ya kata au postikodi.
“Jamii inapaswa kutambua kuwa postikodi ni utaratibu wa kitaalam unaotumika kutenga maeneo ya makazi wakati amwani za makazi ni miundombinu ambayo Kwa Pamoja inatambulisha mahali halisi mtu ama kitu kilipo,aina hii ya utambulisho inaundwa na vitu vikuu vitatu ambavyo ni namba ya anwani,jina la barabara na postikodi,”amefafanua
Mkude amesema,ili kupata tija iliyokusudiwa Katika uanzishwaji wa anwani za makazi na postikodi kila mdau wa maendeleo ana jukumu la kutekeleza kujiwekea miundombinu ya mfumo wa anwani za makazi ikiwa ni pamoja na kutambulisha barabara Kwa kutumia anwani za makazi.
Amesema wananchi pia wanapaswa kuwajibika kutoa na kupokea huduma Kwa kutumia mfumo wa anwani za makazi na kuhakiki taarifa za mfumo huo mara kwa mara .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa