December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafanyabiashara waaswa kwenda kujifunza 77

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online

MWENYEKITI wa Jumuiya ya wafanyabiashara soko la Kariakoo Martine Mbwana amewaasa wafanyabiashara kwenda kwenye maonesho hayo kujifunza kwa kwa wengine ili waweze kuboresha biashara zao na kuendelea kufanya vizuri katika eneo hilo.

Aidha amewaasa kufika katika banda la Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili waweze kuona shughuli za TRA na kuhudumiwa kama wana changamoto zozote.

Mbwana ameyasema hayo katika maonesho ya Kimataifa ya 48 Biashara (sabasaba) jijini Dar es Salaam wakati akozungumza na waansishi wa habari alipotembelea banda la TRA.

“Mimi nimekuja hapa,nimetembelea kwenye banda la TRA,wamejipanga vizuri kuwahufumia wananchibhususan wafanuabiashara 

“TRA wapo idara zote wanafundisha ,wanajibu na changamoto zote zinazohusiana na TRA zinatatuliwa hapa hapa kwenye maonesho.