December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafanyabiashara Kata ya Majohe wailalamikia ofisi ya Serikali Mtaa wa Viwege

Na David John, TimesMajira Online

BAADHI ya wafanyabiashara wanaofanya biashara zao kata ya Majohe wilayani Ilala wameilalamikia ofisi ya serikali ya mtaa wa Viwege kushindwa kuwapanga wafanyabiashara kwenye Soko lililojengwa na serikali kwa kushirikiana na Mwekezaji ndani ya kata hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya kamati ya soko hilo mbele ya waandishi wa habari sokoni hapo Ame Juma Ame amesema licha ya rais Samia Suluhu Hassan kutoa Agizo la kupangwa kwa wafanyabiashara ili wafanye biashara zao pasipo bugudha lakini bado changamoto ipo kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwepo kata ya Majohe,mtaa wa viwege.

Ame amefafanua kuwa hali kukosekana kwa wafanyabiashara kwenye soko hilo ni changamoto kubwa ukizingatia soko limejengwa kwa gharama kubwa jambo ambalo linakatisha tamaa hata kwa wawekezaji.

Wamesema kamati ya soko hilo wamefika hadi ofisi ya mkuu wa mkoa nakuagiza watendaji kushughulikia changamoto hiyo lakini hadi kufikia leo soko hilo maalufu kwa mpemba halina wafanyabiashara kabisa.

Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa viwege kata ya majohe Amina Rashid Kapundi akizungumzia soko hilo Amesema viongozi wa mkoa walimpa majukumu ya kuwaondoa wamachinga pembezoni na kuwaweka sokoni. Lakini changamoto anayoipata wengi wao wameweka magenge kwenye majumba yao.

Amesema kuwa kutokana na hali hiyo inakuwa ngumu kuwabomolesha nakuhusu tuhuma za kukwamisha wafanyabiashara kuingia sokoni amesema si kweli lakini changamoto iliyopo ni magenge ya biashara kuhamia kwenye mabaraza ya wenye nyumba.

Kwaupande wake Afisa Masoko Halmashauri ya jijiji la Ilala Victor Rugemarila tulijalibu kuwatoa ili waingie sokoni. Lakini kuna ukakasi kutoka kwa viongozi wa mtaa kushindwa kuwatoa kwani wao ndio watu wao

Amesema kuwa nivema wakashirikiana ili kuleta tija lakini kubwa kuna hali ya siasa japo yeye alielekeza pawekwe bango kubwa lakuonyesha uwepo wa soko hapo napia wanampango kupeleka gurio kwenye eneo hilo.

“Muda wowote kuazia sasa gurio litaaza na baada ya hapo anahakika kwamba soko litachangamka na katika hili wamejaribu kufanya hivyo kwenye maeneo tofauti tofauti. Victor Rugemarila

Bango linaloonyesha uwepo wa soko mtaa wa Viwege kata ya Majohe ambapo hata hivyo kamati inalalamikia kukosekana kwa wafanyabiashara sokoni