Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa wito kwa wadau mbalimbali kutembelea kwenye banda lao lililopo ndani ya Maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa sabasaba ili kufahamu kazi na miradi inayotekelezwa na shirika hilo ikiwemo mradi mkubwa wa Samia housing Scheme ambao ni mradi wa takribani nyumba elfu 5000.
Mradi huo wa Samia housing Scheme ambao utajengwa Dar es Salaam, Dodoma na mikoa mingine na kwa awamu ya kwanza ya ujenzi tayari umeshaanza eneo la kawe Dar es salaam na zitajengwa nyumba takribani mia 560 kati ya nyumba hizo zitakuwa za vyumba vitatu, viwili na nyumba ya chumba kimoja.
Akizungumza na TimesMajira baada ya kufika katika banda la NHC kwenye maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa Jasson Ipyana amesema wadau na watanzania mbalimbali waje ili waweze kujua fursa za uwekezaji na kazi zinazotekelezwa na shirika.
Aidha, Ipyana amesema muitikio ni kubwa tofauti na miaka ya hapo iliyopita hata idadi imekuwa kubwa kwa watanzania kutaka kujua kazi ya shirika na miradi mbalimbali, hivyo natoa wito kwa wananchi kuendelea kutembea kwenye banda la NHC kwa sababu fursa sni nyingi.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua