Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM
Kwa mara nyingine Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekutana na Wadau wa Maendeleo jijini Dar es Salaam kuwapitisha, kujadili na kupokea maoni juu ya Rasimu ya Sera na mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 na Rasimu ya Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu.
Akizungumza katika kikao kazi hicho, Waziri wa Elimu Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara itaendelea kushirikiana na wadau hao katika kuhakikisha mageuzi ya elimu yanayofanyika yanafanikiwa.
“Mageuzi haya tunayofanya yanahitaji rasilimali katika kuyafanikisha, tuendelee kushirikiana ili yaweza kufanikiwa nasi tutaendelea kuwashirikisha katika kila hatua”,amesema Prof. Mkenda
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Carolyne Nombo amewashukuru wadau hao kwa namna wanavyoendelea kufadhili miradi ya elimu yenye lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo ya Elimu ambae pia ni Mkuu wa Sekta ya Elimu UNESCO Faith Shayo ameipongeza Serikali kwa mageuzi makubwa yanayofanyika kwenye elimu huku akiishukuru Wizara kwa kuwashirikia katika hatua mbalimbali kuelekea mageuzi hayo.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria