Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MAMLAKA ya Serikali Mtandao (e-GA) inatarajia kufanya kikao kazi chake jijini Arusha huku mgeni rasmi katika kikao kazi hicho akitarajiwa kuwa ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama .
Akizungumza leo Februari 6,2023 na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusiana na kikao kazi hicho kitakachofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Benedict Ndomba amesema,takriban wadau 1000Â wa serikali Mtandao wanatajiwa kushiriki kikao hicho kutoka mashirika na taasisi za Umma.
Mhandisi Ndomba amesema lengo la kikao kazi hicho ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Seeikali Mtandao ili kujadiliana mafanikio ,changamoto pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya kukuza Serikali Mtandao nchini ili kuhimiza matumizi sahihi na salama ya TEHAMA sambamba na kuboresha utendaji kazi katika Taasisi za Umma na utoaji w a huduma bora kwa wananchi.
Aidha amesema kikoa hicho cha tatu kitaongozwa na kaulimbiu isemayo’Mifumo Jumuishi ya Tehama,kwa utoaji huduma bora kwa umma’ iliyolenga kuhamsisha taasisi za umma kutumia mifumo Jumuishi inayowasiliana katika utendaji kazi kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Mhandisi Ndomba ametumia nafsi hiyo kuelezea baadhi ya mafanikio ya e-GA ambapo amesema kuwa ni pamoja na kusimamia uzingatiaji wa sera,sheria na miongozo ya serikali Mtandao kwa taasisi za umma ,kuwezesha usanifu na ujenzi wa mifumo ya Serikali Mtandao ya kitaasisi nay a kisekta ili kuboresha utoaji huduma kwa umma.
Mafanikio mengine ni kuboresha na kuongeza mawanda ya kusimamia uendeshaji wa miundombinu shirikishi ya serikali Mtandao,kutoa msaada wa kiufundi kwa Taasisi za umma katika matumizi sahihi na salama ya huduma za serikali Mtandao.
Aidha Mamlaka ya Serikali inawakumbusha wadau wote wa TEHAMA hapa nchini kushirikiki kamilifu kikoa cha tatu cha e-GA kwa kufanya usajili kupitia mfumo wa TSMS .
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best