December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wadau maonesho ya sabasaba ya 47 waisifu TanTrade

Na David John,Timesmajiraonline.

MKURUGENZI mweza wa kampuni ya masoko nchini (TanzaKwanza) Francis Mlacha amesema kuwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) katika kuelekea maonesho ya sabasaba mwaka huu wanafanya jambo muhimu la kuwaita wadau na kuelezea maandalizi ya namna walivyojipanga kushiriki maonesho hayo.

Amesema kuwa TanTrade wamekuwa wakiita wadau mbalimbali ili kuzungumzia maandalizi na namna walivyojipanga katika kuhakikisha kwamba maonesho ya sabasaba mwaka huu yanakuwa ya kukumbukwa na yanavutia zaidi wawekezaji ,watoa huduma pia wateja na wao kama Tanzakwanza wanashirikiana naTantrade kuandaa mabanda maalumu.

Mlacha ameyasema hayo Mei 2 mwaka huu kwenye ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TanTrade katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maonesho ya kimataifa ya 47 ya sabasaba ambayo yanatarajia kuaza Juni 28 kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa wilayani Temeke .

” lengo kubwa ni kuweza kuonesha huduma na bidhaa mbalimbali zinazopatikana Tanzania,tumezingatia wito wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hasaan ambao alitoa mwaka jana aliposema sekta nane za kimkakati zikutane na wadau kutoka sekta binafsi lengo nikuziweka sekta hizo nane ikiwemo ,sekta ya Madini,kilimo ,Tehama ,?Mazingira,maendeleo ya vijana ,Sanaa na michezo.”Amesema

Nakuongeza kuwa “Leo hii tutoe wito Kwa wadau ambao wapo katika sekta hizi wawasiliane na Tanzakwanza ili waweze kuwa sehemu ya sabasaba exerple village lakini pia lengo la mabanda haya kuwakutanisha wadau sekta binafsi na (potetional investors) ambao wameshawaalika zaidi ya mabaraza ya Biashara 123,.”Amesema Mlacha.

Amefafanua kuwa yapo mataifa kadhaa ambayo yamethibitisha kushiriki katika maonyesho hayo hivyo lengo lao ni kuwakutanisha pamoja na lengo la pili kufanya forum maalumu ambapo watajadiliana fursa na changamoto mbalimbali ambazo zipo katika sekta hizo nane.

Ameongeza kuwa jambo la mwisho nikwamba wanalenga kutambua mchango wa wafanyabiashara na makampuni ambayo yamefanya vizuri katika sekta husika labda kwenye sekta ya madini ni akina nani ambao wamefanya vizuri Kwa mwaka mmoja uliopita na vigenzo vitaandaliwa na mamlaka husika.

Lakini pia malengo makubwa kabisa ni kuhakikisha kwamba suala la uwekezaji linakuwa sio wimbo tu wataifa bali wanavutia wawekezaji wa ndani na nje kwasababu Serikali inafanya vizuri na inafanya vizuri kwenye diplomansia ya uchumi hivyo wanaungana na TanTrade Kwa kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania.

Naye profesa Dorcas E. kibona Mwazilishi na mtendaji wa kampuni ya Dorkin Organic Akizungumzia maandalizi hayo ya sabasaba mwaka huu Amesema kuwa Yeye kama mtafiti na mgunduzi wa chakula cha asili wamejipanga sawa sawa na alipo mama nao wapo.

Amesema wao wanajishughulisha na kilimo hai ambacho hakitumii madawa ya Viwandani ni kilimo ambacho kinalinda uhai wa mwanadamu na chakula hicho mwanadamu akila anakuwa salama na ndio maana Dorkin wanekuja na mnyororo wa thamani kuazia kwenye udongo, mbegu,kuchakata ,kufungasha na kumpa mlaji chakula chenye uhai.

Amesema ndio Kampuni pekee ambayo imeweza kufanya vizuri na wamefurahia sana TanTrade Kwa mwaka huu wameweza kuendeleza kutoa mwelekeo wa sabasaba Kwa mwaka huu na hakuna shaka habari za maandalizi yake zinaenda mbali zaidi na wao kama Dorkin matarajio yao nikwenda kuwapa watanzania kilicho Bora kabisa.

Katika mkutano huo pia alikuwepo Mwenyekiti wa wamachinga mkoa wa Dar es Salaam Namoto Yusuph na msanii wa senema hapa nchini Salim Mohamed maalufu (Gambo zee Gamba ) ambapo kwa pamoja wameelezea walivyojipanga kuelekea sabasaba ya mwaka huu huku wakitoa wito Kwa watanzania kushiriki kikamilifu kwasababu kutakuwa na vitu vya tofauti.