October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wabunge wawili CHADEMA waingia rasmi CUF

Na Irene Clemence

ALIYEKUWA Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Wilfred Rwakatale pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kigoma, Sabriana Sungura wamejiunga rasmi leo na Chama cha Wananchi CUF.

Aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Wilfred Rwakatale akipokelewa na wanachama wa chama cha CUF mapema leo.

Wakizungumza jijini Dar es Salaam leo baada ya kupokelewa na wanachama wa CUF katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, Lwakatale amesema ameamua kurudi nyumbani,kwani yeye ni muhasisi wa muda mrefu.

Amesema, Chama Cha Wananchi (CUF) kimemfuta machozi na kumpa nguvu,hivyo yupo tayari kusimama imara na kufany kazi kwa ushirikiano.

“CUF mmenifuta macho na kunipa nguvu tarehe 5 Juni nitakwenda Bukoba nikiwa nimetunisha kifua mbele,”amesema Lwakatale. Pia aliwaomba radhi wanaCUF wote aliowakosea na kudai kuwa yeye amewasamehe waliomkosea.

Aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatale akiwasili katika ofisi za Chama Cha Wananchi CUF Buguruni jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Irene Clemences).

Aidha, amewataka wanachama CUF kusimama imara ikiwa ni pamoja na kuangalia ni wapi chama hicho kimekuwa kikikwama. Vilevile amrsisitiza kuwa sio vyema kugombania madaraka katika chama kwani mambo hayo ni ya muda mfupi tu.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu Kigoma, Sabriana Sungura amesema ameamua kujiunga na chama hicho kwa lengo kupata haki sawa na furaha baada ya kuikosa kwa muda mrefu katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA.

Amesem, katika chama hakukuwa na haki wala furaha badala yake kilitawaliwa na ubinafsi pamoja umimi.

” Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimetawaliwa na ubinafsi pamoja na umimi,kwani baada ya kufunga ndoa na mtu anayetoka katika Chama Cha Wananchi CUF nilinuniwa pamoja na kutegwa kwa madai kuwa natoa siri za chama,”amesema Sabrina.

Amesema kuw, baada ya kuona hayo moja kwa moja kwa imani yake aliona jambo hilo ni la ubinafsi na kuamua kutazama pembeni.

Naye Makamu Nwenyekiti wa CUF Bara, Maftah Nachuma, amesema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinashika dola pamoja na kurudisha heshima iliyokuwepo awali.

Amesema,ujio wa wabunge hao ni mzuri na umelenga kukifikisha Chama Cha CUF mbali kwa kuhakikisha itikadi ya haki sawa kwa wote inatekelezwa.

“Chama Cha CUF kimezaliwa upya Sasa kwa pamoja tunashiriki na kusimama imara kuhakikisha chama kinasonga mbele,”amesema Nachuma.