November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wabunge wa CHADEMA, Pascal Haonga na Joseph Haule wakiingia katika viwanja vya Takukuru jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa

Wabunge wanaohama Chadema wanadanganya umma

Na Joyce Kasiki, TimesMajiraonline, Dodoma

MBUNGE wa Mbozi Pascal Haonga amesema,wabunge wanaohama chadema na kwenda vyama vingine waache kuudanganya umma kuhusu makato ya wwbunge ambayo yapo kikatiba kwa ajili kukijenga chama.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhojiwa nabtakukuru leo jijini Dodoma Haonga amesema,wabunge hao wabakwenda kwenye vyama vingine na kuudanganya umma wakati wwnajua suala lile lipo kikatiba.

“Wabunge hawa wana nia ovu dhidi ya chadema,tunajua wabunge hawa wana nia ovu ya kukisambaratisha chama na ninapenda kuwaambia katika chama tulianza na Mungu na tutanaliza na Mungu,” amesema na kuongeza

“Swali la kujiulizq kwa nini hili liibuke saa hizi wakati alishasoma katiba na aliielewa ,sasa anapoanza kutoka kwenda vyama vingine ndio anaanza kulalamika .”

Kwa upande wake Mbunge wa Mikumi Joseph Haule amesema,makato ya chama yaliyoleta utata yapo katika katiba ya chama hicho Ibara ya 7(a)na 7(b) na kila mbunge alitoa fedha hiyo kwa mujibu wa katiba.


Amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kukijenga ambapo mbunge wa Jimbo anakatwa asilimia 10 na Vito maalun anakatwa asilimia 30 ya mapato yake.