December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wabunge waitaka Serikali kuongeza mkataba wa SONGAS

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wabunge Mbalimbali wakati wakijadili Bajeti ya Wizara ya Nishati Leo Bungeni wameitaka Serikali Kuongeza Mkataba wa Kampuni ya kuzalisha Umeme ya SONGAS.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu amesema Kampuni hiyo inapaswa kuongezewa mkataba kwa sababu inafanya kazi nzuri ya Kuzalisha Umeme wa Uhakika na kulipunguzia Mzigo Shirika la Umeme Nchini TANESCO huku akisisitiza SONGAS ni mfano bora wa matokeo ya ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, yaani PPP.