Na John Bera, TimesMajira Online
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja ametoa wito kwa wafanyabiashara na wamiliki wa makampuni mbalimbali hapa nchini kuunga mkono juhudi za Serikali za kutangaza utalii na vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini kupitia biashara zao.
Masaanaja ametoa wito huo leo jijini Mwanza wakati wa maonesho ya Biashara ,Uwekezaji na Utalii yanayowahusisha wadau mbalimbali.
Amesema, wafanyabiasha ni wadau wakubwa wa utalii hivyo wana nafasi kubwa ya kuutangaza utalii hatua itakayosaidia kuongeza idadi ya watalii.
“Nawaomba sana ninyi wafanyabiashara, kupitia makampuni yenu mtangaza Utalii wa Tanzania na vivutio vyake,ninyi ni wadau wakubwa wa utalii,”amesema Mary Masanja.
Amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa wanapaswa kutambua kuwa Sera ya Tanzania ya Viwanda itaendelea kutekelezwa kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekua akiwasisitiza Watanzania wawekeze katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo alisema wafanyabiashara wakishirikiana vizuri wataweza kukuza uchumi wa nchi pia kuutangaza utalii.
Aidha, amesema Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali ikiwemo uondoaji wa urasimu na ukiritimba kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza hapa nchini.
“Serikali tunaendelea kuziondoa changamoto kuziondoa changamoto zote zinazolalamikiwa na wafanyabiasha na wawekezaji,tuvute subira kidogo haya mambo yatakwenda kurekebishwa vizuri,”alisema Mashimba.
Hata hivyo, alizitaka mamlaka za Serikali za mitaa kutengeneza wafanyabiashara watakaolipa mapato kwa kuwapatia maeneo watakayofanyia biashara ili waweze kulipa kodi na kukuza uchumi wa nchi.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja