Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani la WoteSawa limetoa vyeti kwa waandishi wa habari 7,mkoani Mwanza kwa kutambua mchango wao katika kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya masuala yanayohusu wafanyakazi wa nyumbani.
Akizungumza wakati wa utoaji vyeti hivyo wakati wa shirika hilo likiadhimisha siku ya kimataifa ya Wafanyakazi wa nyumbani Juni,16,2023Ofisa Msimamizi wa Makao na Uwezeshaji wa WoteSawa Demitila Faustine, ameeleza kuwa wameona watoe vyeti hivyo kwa waandishi hao wa habari kama hamasa ya wao kuendelea kupaza sauti za wafanyakazi wa nyumbani.
Demetila amesema pia waandishi hao waendelee kuwahamasisha wafanyakazi wa nyumbani pamoja na kuweza kuendelea kuifanya jamii ifahamu haki na mambo muhimu na msingi ya kuzingatia kwa maslahi ya wafanyakazi wa nyumbani.
“Tunawashukuru waandishi hao kwa kazi waliofanya,pia tutaendelea kuwahamasisha wazidi kuandika masuala yanayohusu wafanyakazi wa nyumbani ili kuifikia jamii na kuihabarisha na kuelimisha juu ya masuala yanayohusu wafanyakazi hao,”amesema Demitila.
Akizungumza mara baada ya kupokea vyeti hivyo mmoja wa waandishi wa habari hao Sada Amir, ameshukuru shirika hilo kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari juu ya kuhabarisha na kuelimisha jamii kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo ya wafanyakazi wa nyumbani.
Miongoni mwa waandishi wa habari walio tunukiwa vyeti hivyo vya kutambua mchango huo ni Judith Ferdinand mwandishi wa gazeti la majira na timesmajira online kwa Mkoa wa Mwanza,Sada Amir kutoka gazeiti la Mwananchi,George Binagi kutoka BMG Online na Alloyce Nyanda kutoka Star TV.
Wengine ni Moses Methew- TBC, Sada Amir- Mwananchi,Deus Gabon- Kwizera FM na Sharifa Suleiman- RFA.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â