Na Penina Malundo, timesmajira
WAANDISHI wa habari takribani 30 kutoka mikoa mbalimbali nchini wamepatiwa mafunzo ya kuandikq habari za ukweli na kuhakiki vyanzo sahihi kuhusu habari hizo.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Afrika Check Alphonce Shiundu katika mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Nukta Afrika.
Mara baada ya mafunzo hayo, Shiundu amesema lengo la mafunzo ni kitambua habari za uongo zinazochapishwa
kwenye mitandao ya kijamii na kuzua taharuki, hivyo ni vyema jamii ikatambua kuhusu habari za uzushi.
Shiundu amesema, taasisi yao imekua okitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika ili waweze kitambua habari za ukweli.
“Tumetoa mafunzo juu ya uelewa wa habari za kweli kwa wanahabari hawa, kwa lengo la kujifunza njia mbalimbali za kuthibitisha habari za kweli,” amesema.
Hata hivyo Shiundu amesema, baadhi ya watu wamekuwa wakisambaza taarifa za uzushi kwa makusudi huku wengine wakisambaza bila ya kujua.
“Masomo haya ya fact-cheking ni muhimu kwa waandishi wa habari pamoja na vyombo vyenu, mtakuwa wataalamu kuhakikisha habari mnazotoa ni za ukweli ziwe za picha au video,” amesema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mafunzo kutoka Nukta Afrika, Daniel Mwingira aliwashukuru Afrika Check kuja nchini na kutoa mafunzo haya kwa waandishi wa habari. Hivyo ni jambo la kuwashukuru kwa kutuamini na kutusaidia Tanzania,” amesema na kuongeza.
“Tunaamini mlichojifunza ndani ya siku mbili mmekichukua na mnaenda kukifanyia kazi. Hii itakuwa njia moja wapo ya kuyapa mafunzo haya uzito unaostahili kwa kuona mlichojifunza mtakifanyia kazi,”.
Naye mmoja wa waandishi aliyepata mafunzo hayo, Maulid Mbaga amesema kupitia mafunzo hayo amejifunza vitu vingi vya aundikaji habari za ukweli.
“Tunawashukuru Nukta Afrika kwa kushirikiana na Afrika Check juu ya mafunzo haya mazuri na muhimu sana kwetu ambayo yatatusaidia kuhakikisha tunaepusha habari za uzushi ambazo huwa zinasambaa katika mitandao ya kijamii kutokanq na kukua kwa technologia,” amesema na kuongeza.
“Mafunzo haya yatatusaidia kujua namna gani ya kuepuka habari za kizushi na nini tufanye ili tuweze kufikisha kitu ambacho ni cha kweli,” amesema.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato