Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Waandishi wa habari wametakiwa kutokata tamaa katika utendaji kazi wao badala yake wazingatie weledi,sheria na kanuni kuhakikisha wanatoa kitu kilicho bora kinachomfaa mlaji pamoja na kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Yuhoma Educational Limited Yusuph Yahaya wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea ofisini kwake kwa ajili ya kueleza mipango na shughuli za taasisi hiyo ikiwa ni wiki ya wadau wa habari kutembelewa na waandishi wa habari ambao ni wananchama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza(MPC).
Ambapo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika hafla ya usiku wa wadau wa habari Kanda ya Ziwa na waandishi wa habari iliondaliwa na MPC kwa udhamini wa wadau mbalimbali itakayofanyika Octoba 20,2023 jijini Mwanza.
Yahaya ameeleza kuwa waandishi wa habari wahakikishe wanacho kitoa kinamfaa mlaji na wasimame kwenye haki ili waisaidie serikali.
“Tumieni muda mwingi kumsaidia Rais wetu Samia ana lengo zuri lakini hawezi kumfikia kila Mtanzania kwa kueleza sera za maendeleo ila kupitia nyingi mnaweza kupeleka ujumbe,fikiria mkiamka mkasema amuandiki habari maana yake mmetuzimia umeme,”ameeleza Yahaya na kuongeza kuwa
“Waandishi wa habari mna silaha ambazo ni karatasi,kalamu,kamera na vitu kama hivyo mnapotamfuta mkate wenu wa kila siku tambua kuwa mpo vitani haijalishi vita inayoonekana au isiyo onekana kikubwa katika maisha ambayo nimepata ujuzi katika Ukurugenzi ni kutokukata tamaa,malipo yenu yanaweza yasiwe hapa lakini huko mbeleni tunakoenda mkayaona,”ameeleza Yahaya.
More Stories
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19
Wananchi Kiteto waishukuru Serikali,ujenzi wa miundombinu ya barabara