December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania.Leah Ulaya

Waalimu ni kundi kubwa linalohitaji utulivu na weledi mkubwa

Na Penina Malundo

RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania.Leah Ulaya amesema kundi la walimu ni kundi kubwa linalohitaji utulivu na weledi mkubwa katika utendaji wao wa kazi.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania unaofanyika uwanja wa Jamhuri Dodoma. Amesema wanamuhaidi Rais Magufuli kuwa wataendelea kuwa watulivu kipindi chote kwani Rais Magufuli amekuwa mtetezi wao siku zote.

Amesema licha ya kuwepo kwa ugonjwa wa Corona na kufungwa kwa shule lakini Rais Magufuli hajasitisha misharaha yao hii inaonyesha ni namna gani Rais huyo anavyowajali.

“Takribani miezi miwili au mitatu juu ya kufungwa kwa shule lakini Rais Magufuli ujasitisha mishahara yetu tunaamini unastahili sana,” alisema na kuongeza

“Walimu tunakuhaidi kufanya kazi kwa bidii ,weledi mkubwa, kuwa wazalendo na kuwa mstari wa mbele katika kupigania nchi yetu,” alisema